Wewe ni mwanadada mrembo na mwenye roho nzuri - Otile amsherehekea Nabayet

Mapema mwaka huu Otile Brown na Nabayet walitangaza kuvunjika kwa mahusiano yao baada ya kudumu kwa takriban miaka 3.

Muhtasari

• Wawili hao walitengana mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miaka mitatu.

• Walipoachana, Brown alikuwa amesema kuwa hata watakapoachana bado ataendelea kumheshimu na kumjali Nabbi.

OTILE // NABBI
Image: OTILE IMSTAGRAM

Mwanamuziki Otile Brown ameamsha gumzo miongoni mwa mashabiki wake baada ya kuchapisha picha ya aliyekuwa mpenzi wake Nabayet almaarufu Nabbi.

Brown alichapisha picha hiyo akiwa amemwandikia Nabbi ujumbe mfupi wa kumtakia maisha marefu yenye furaha..

"Heri ya kuzaliwa kwa mwanadada mrembo zaidi na mwenye roho nzuri ninayejua Nabayet,"alisema.

Nabbi amejibu na kumshukuru Otile kwa ujumbe huo na kwa kumtakia maisha mema na kusema kuwa anamthamini mwanamuziki huyo.

Wawili hao walitengana mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miaka mitatu.

Walikuwa na mapenzi ya kutokuwa karibu na mpenzi wako kwa sababu Nabbi alikuwa nchini Ethiopia wakati huo.

Walipoachana, Brown alikuwa amesema kuwa hata watakapoachana bado ataendelea kumheshimu na kumjali Nabbi.

Alisema kuwa mpenzi huyo wake wa kitambo ni mtu mzuri na kwa hilo bado ataendela kuwa na uhusiano mzuri naye.

"Namtakia mema anaposonga mbele,"alisema.

Wakati huo huo,Brown alifichua kuwa mara yake ya mwisho kuwa na Nabbi, walikuwa wanajaribu kutafuta mbinu ya kuurekebisha uhusiano wao ila hatimaye waliamua kuukatiza uhusiano huo.

Picha hiyo aliyoiweka Otile Brown imezua madai ya kuwa wamerudiana na Nabbi.