Mwanasosholaiti mstaafu Vera Sidika amejipata kwenye dimbwi la kurushiwa matusi baada ya kugundulika kuwa alikuwa anafukuzia kiki kwa ajili ya kutoa ngoma yake mpya.
Mwanadada huyo Ijumaa aliachia kibao chake kipya kweney ukurasa wake wa YouTube kwa jina Popstar na kwa kuitizama video ile kwa umakini wa jicho la tatu mtu anaweza sema kuwa Sidika bado yupo na lile umbo lake lenye makalio makubwa.
Masimango yanamwandama haswa baada ya kupakia picha wiki hii akitania wanamitandao kuwa alifanya upasuaji wa kupunguza makalio yake kutokana na sababu za kiafya.
Katika picha hiyo ambayo ilizua gumzo pevu kwenye mitandao ya kijamii, Sidika alieleza kwa mapana kuwa alilazimia kutafuta suluhu baada ya kupitia changamoto nyingi za kiafya kutokana na kile alisema kuwa ni kufanay upasuaji awali wa kuongeza makalio, upasuaji ambao ulimwendea mrama.
Aidha, Sidika aliwashauri wanadada kujikubali jinsi walivyo na kukoma kabisa kutafuta huduma za upasuaji ili kuongeza makalio yake, akisema kuwa ni hatari na yeye alinusurika kifo.
Baada ya kuona video hiyo, wengi wamemsuta Sidika kwa kusema kwamba aliwapotezea muda wao kumzungumzia kutokana na ile picha iliyomuonesha akiwa na makalio yaliyopunguka kwa kiasi kikubwa,
Wengi walisema kuwa picha ile haikuwa yake halisi bali aliifanyia uhariri wa kidijitali almaarufu photoshop kwa kimombo.
Wengine walilalama vikali kwa kusema kwamba hata kwenye mitandao yake sasa baada ya kuachia wimbo amefungika kitufe cha kutoa maoni na kumtaka aweke huru ili waweze kumsuta ndio angalau hasira zao zipoe kwani aliwahadaa na kutrend mitandaoni kwa njia ya kurubuni.