logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Wasanii wa kike wamelala,'Eric Omondi asema huku akimsifu Vera Sidika

Zaidi ya yote mchekeshaji huyo alidai kwamba wasanii wa kike nchini wamelala

image
na Radio Jambo

Burudani09 October 2022 - 19:34

Muhtasari


  • Dakika chache zilizopita Eric Omondi alivunja ukimya kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mmoja wa kipenzi na mshawishi wa mitndao nchini Vera Sidika

Dakika chache zilizopita Eric Omondi alivunja ukimya kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mmoja wa kipenzi na mshawishi wa mitndao nchini Vera Sidika.

Eric Omondi ametoa matamshi yake kuhusiana na Vera Sidika ambaye amevuma mitandaoni baada  ya upasuaji wake kuathiri sekta ya burudani.

Kwa mujibu wa Eric Omondi, Vera Sidika ameteka hisia za Wakenya, jambo ambalo Watanzania na Wanigeria wamekuwa wakifanya.

Zaidi ya yote mchekeshaji huyo alidai kwamba wasanii wa kike nchini wamelala, na kwa hivyo wanahitaji kuamka.

"Sijali kile mnafikiria kuhusu Vera Sidika,kile najua chote amefanya tuongee,tumevutiwa na kupata umakini wetu wote PERIOD hivi ndivyo Watanzania na Wanigeria wamekuwa wakipata umakini wetu!!!

Na kisha akadondosha video ya Muziki ya HOOOOT๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ bora kuliko 98% ya kile ambacho Wasanii wa Kenya Hutoa. Hiyo ni SHOWBIZ HAPO HAPO!!!

Alafu the fact that she had the Space to do it simply means watu Wamelala Fofofo, Hasa Wasanii wa Kike wa Kenya Uuuuuuuuuuuuuui๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ™‰๐Ÿ™‰๐Ÿ™‰ @queenveebosset KUDOS๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘."

Mapema wiki hii Vera aliwaacha wanamitandao na mazungumzo baada ya kufichua kwamba alifanyiwa upasuaji wa makalio.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved