logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond ajivunia hatua ya Zuchu kuteuliwa kuwania tuzo za MTV

Zuchu aliteuliwa kwenye tuzo za Kiafrika miongoni mwa wasanii wengine wakubwa

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 October 2022 - 07:01

Muhtasari


• Diamond ameonyesha kujivunia kwa uteuzi huo wa Zuchu kwa kuwa yeye ni msanii aliyesaini kwenye lebo yake ya WCB Wasafi.

• Vilevile, Diamond alikuwa na mshangao baada ya kuzawadiwa na Zuchu kwa kupewa cheni iliyoundwa kutoka kwenye madini ya dhahabu kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa aliyosherehekea wiki mbili zilizopita.

katika ziara yao ya Ufaransa.

Diamond ameonyesha kujivunia kwa uteuzi huo wa Zuchu kwa kuwa yeye ni msanii aliyesaini kwenye lebo yake ya WCB Wasafi.

Mwanamuziki Diamond Platinumz amempongeza Zuchu kwa hatua hiyo yake ambayo aliweza kufanikisha.

Diamond aliwafahamisha mashabiki wake kuwa Zuchu ameteuliwa kwenye tuzo za kifahari za Kiafrika.

Mwanamuziki huyo aliwafahamisha mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram ili  wamesherehekee na kumsaidia kumpongeza kwa ushindi huo.

"Hivi, macho yenu yanaona kama ninavyoona mimi lakini ama?" Diamond alisema huku akifurahia ushindi huo.

Diamond ameonyesha kujivunia kwa ushindi huo wa Zuchu kwa kuwa yeye ni msanii aliyempa mkataba kwenye lebo yake ya WCB Wasafi.

Vilevile, Diamond alikuwa na mshangao baada ya kuzawadiwa na Zuchu kwa kupewa cheni iliyoundwa kutoka kwenye madini ya dhahabu kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa aliyoadimisha wiki mbili zilizopita.

Mwanamuziki huyo alimshukuru Zuchu kwa kumpa zawadi hiyo na kuchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram matukio hayo alipokuwa anazawadiwa.

“Maneno hayawezi elezea shukrani yangu kwa hili Zuuh, nisije nitateleza kuandika waandishi wakapata stori. Ila jua nakushukuru sana na siku zote utaendelea kuwa pale,” Diamond alimshukuru.

Zuchu pia alimshukuru Diamond kwa kumtambulisha kwenye lebo yake na kumfanya kuwa mwanamuziki mkubwa anayevuma na kufanya jina lake liwe kubwa,

Cheni hiyo ilitengenezwa na jamaa mmoja kwa jina Dr Smile kupitia biashara yake ya Shohreh Custom Made.

Mwanamuziki Zuchu amekuwa msanii wa kwanza wa kike wa Afrika Mashariki  ambaye ameteuliwa kwenye tuzo za Kiafrika za mwaka huu.

Ameteuliwa miongoni mwa Burna Boy, Arya Starr, Black Sheriff, Musa Keys na Tems na anawania nafasi hiyo kwenye kipegele cha Best African Act.

Kulingana na runinga ya Wasafi, Zuchu alijitayarisha ipasavyo ili kufanikisha zawadi hiyo kwa kuchukua muda wa miezi miwili kimya kimya na kuzama mfukoni ili aweze kuibuka na kima cha shilingi milioni 29 za Tanzania.

Zuchu aliandika ujumbe wa kuonyesha furaha aliyokuwa nayo kwa kufanikisha tuzo hiyo kwenye mtandao wake wa Instagram

“Tanzania simameni juu, msichana wenu ameteuliwa kuwania tuzo za MTV EMA. Mungu ni mwema, niseme ahsante kwa sababu yenu ndio mimi niko hapa nawapenda sana,” Zuchu aliandika na kuahidi kurejea na maelezo mazuri zaidi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved