Jinsi upasuaji wangu wa matiti ulihasisha watu - Vera Sidika

Sidika alisema kuwa upasuaji wake uliwahamasisha watu na kuwafahamisha kuhusu mchakato huo

Muhtasari

• Alisema kuwa sasa hivi watu wengi haswa wanawake huwa hawaongelei upasuaji huo mabaya  na kuwa wameweza kuiona kama njia nzuri ya kubadlisha umbo.

• Aliongeza kuwa upasuaji huo uliwasaidia wanawake wanaougua ugonjwa wa Saratani ya matiti na kuwatolea hofu ya kukemewa na watu.

Vera Sidika

Vera Sidika alieleza jinsi umbo lake na upasuaji wake wa makalio umewaelemisha watu.

Alisema kuwa upasuaji huo aliufanya wakati watu bado hawakuwa wamefahamu kuwa kuna mchakato wa kuongeza viungo vya mwili.

Licha ya kukemewa alipoonekana mara ya kwanza akiwa na umbo hilo lake, watu waliweza kujua kuwa kuna uwezo wa kuukarabatisha mwili wao.

"Kitu kimoja ninachoweza kusema ni kuwa nilielimisha watu watu wengi kuhusu upasuaji huu wa kimaumbo wakati na sasa karibu kila mtu anaufanya".

Alisema kuwa sasa hivi watu wengi haswa wanawake huwa hawaongelei upasuaji huo kwa ubaya  na kuwa wameweza kuiona kama njia nzuri ya kubadlisha umbo.

Hata hivyo, Sidika alisema kuwa wanawake wengine wamehamasishwa na marafiki zao kufanya upasuaji huo na kuutumia vibaya.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliongeza kuwa baadhi ya watu wanatumia upasuaj huo kwa njia isiyo faa na wanaweza kukutwa na madhara mbalimbali.

"Watu wengi waliohamasihwa kuufanya upasuaji huo hawajui madhara yake, unapata mtu anafanya upasuaji huo anafariki akiwa kwenye mchakato huo ama baadaye anabadilika kabisa," Sidika alisema.

Aliongeza kuwa upasuaji huo uliwasaidia wanawake wanaougua ugonjwa wa Saratani ya matiti na kuwatolea hofu ya kukemewa na watu.

"Upasuaji huu ulipotokea ulikuwa kwa ajili ya kuzuia huzuni miongoni mwa wanawake ambao wamekuwa na saratani ya matiti na ni mchakato ambao ni bora kabisa," mwanansosholaiti huyo aliwafahamisha watu.

Sidika alisema sababu yake ya kufanyiwa upasuaji huo ni kuwa alihisi mwili wake haukua na usawa, alikuwa amebarikiwa na makalio ila matiti yalikuwa madogo.

Aliongeza kuwa mtu akiwa na umbo zuri hawezi kuwa na tashwishi yoyote na umbo lake na kuwa hawezi kushinikizwa kujibalisha.