Kuna mtu alituacha na sasa anatuchukia - Vivian aeleza sababu ya kuwa na huzuni

Vivian amedokeza kuwa hajakuwa sawa kwa muda sasa

Muhtasari

• Alisema kuwa amekuwa akijaribu kuwa sawa kwa muda sasa ila hajaweza kuwa na mafanikio kutokana na kisa hicho.

Hapo awali kulikuwa na fufunu mtandaoni kuwa Vivian alitengana na mepnzi wake Sam West ila bado mwanamuziki huyo hajafahamisha watu wala kufichua kama madai hayo ni ya kweli.• 

Mwanamuziki Vivian

Mwanamuziki Vivian amefichua kukabiliana na msongo wa mawazo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Vivian alisema sababu yake ya kuwa na msongo wa mawazo ni kuwa anapitia wakati mgumu kwa kuwa amempoteza mtu muhimu kwenye maisha ayake.

Alisema kwamba amekuwa akijaribu kuishi maisha ya kawaida kwa muda sasa ila hajaweza kurejelea hali yake ya awali. 

Mwanamuziki huyo aliongeza kuwa amekuwa akijishirikisha na  mambo aliyodhani yatamwezesha kurudi kwenye hali yake ya furaha.

Hata hivyo, mama huyo hakutaja alichokuwa anajishirikisha ama kufanya ili aweze kuwa kwenye hali shwari.

"Sijakuwa nikijihisi sawa. Nimekuwa nikipata msaada ila wakati mwengine huwa sijiwezi na najikuta nikirudi kwenye msongo wa mawazo. Moyo wangu umekuwa mzito," mwanamuziki huyo aliwajulisha mashabiki wake.

Vivian alisema kuwa moyo wake umekuwa ukikereka kwa huzuni na hii ni ndio mara ya kwanza kuwa katika hali hiyo. 

Mwanamuziki huyo hakufafanua ni nani aliondoka na kumuacha katika hali ya upweke.

Vivian alieleza kuwa maisha bila mtu huyo ni hali inayompa msongo wa mawazo asiyoweza kuhimili maishani.

"Kuna mtu ambaye alituacha na kwa sasa anatuchukia. Nimejaribu kujijenga na kujirudisha kwenye hali yangu halisi ila nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na kuwaza ni kwa nini niko kwenye hali hii," Vivian alieleza.

Aliwaomba watu kumweka kwenye maombi ili aweze kuwa mtu bora bila msongo.

Vivian alisema kuwa yeye bado ni mama wa mtoto wake anayehitaji kuwa na malezi bora na wakati wa sasa ambapo hajiwezi anahitaji mashabiki wake wamweke kwa maombi.

Mwanamuziki huyo alikanusha madai ya kuwa anatafuta kiki na kusema kuwa huo ni mchezo wa wanamuziki wengine si yeye.

"Sio kiki bali ni suala tu la kibinadamu linalozungumziwa. Suala hilo la kiki lishindwe katika jina la Yesu," Vivian alimjibu shabiki huyo.

Hapo awali kulikuwa na fufunu mtandaoni kuwa Vivian alitengana na mpenzi wake Sam West ila bado mwanamuziki huyo hajawafahamisha watu wala kufichua kama madai hayo ni ya kweli.