logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bibi Harusi atemwa baada ya bwana harusi kugundua ana watoto 4

''Bibi harusi hakuniambia, tayari ana watoto wanne kwenye ndoa ya hapo awali"  - Bwana harusi alisimulia.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 October 2022 - 13:54

Muhtasari


  • • Mwanamke alijitupa miguuni mwa mwanaume huyo akiomba amsamehe kwa kutomtaarifu kuwa alikuwa na watoto 4 na bado anampenda.

Siku ya maharusi wakifunga pingu za maisha huwa siku yenye bashasha na nderemo nyingi kusherekea wanapoingia maisha mengine.. Siku hii huwa yenye kupangwa ikapangika.

Ila kunayo harusi humo nchini Nigeria ambayo ilisherehekewa kwa vilio na majuto ya mjukuu, baada ya bibi harusi kuonekana akilia kwa nguvu huku wanawake wenzake wakijaribu kumliwaza.

Kizazaa hiki kilijili kwenye barabara kuu na watu walipoulizwa kinachoendelea, bwana harusi alisema:

''Bibi harusi hakuniambia, tayari ana watoto wanne kwenye ndoa ya hapo awali" 

Klipu hiyo iliwafanya walioitazama kumpa pole  Bi. harusi kwa jinsi ambavyo mwanamke huyo alijitupa miguuni mwa bwanake mtarajiwa kumhimiza asimwache lakini ombi lake likagonga mwamba.

Ila wanamtandao wengi walisema mwanamke huyo hastahili kuonewa huruma kwa sababu halikuwa jambo la busara kuficha habari muhimu kama hiyo kutoka kwa mwanamume ambaye alitaka kuolewa naye.

 “Kwa nini asimwambie mwanamume kabla ya harusi.? Yeye ni mdanganyifu kwenye ndoa, lakini naomba Mungu amrehemu." mwanamitandao mmoja alisema.

"Mke angemwambia kabla ya harusi hiyo inamaanisha kuwa anamficha mengi na hiyo ni hatari." Mwanamitandao wa pili alisema.

''Kama hadithi ni ya kweli  sifai  kumlaumu kijana hata kidogo… Mbona hukumwambia hata siku moja. Jipe moyo lakini dada yangu'' Mwanamitandao mwingine alionesha kujali.

''Kama yeye sio mtu wa kufunguka...Hataona mwanamume yeyote wa kumuoa'' 

''Tafadhali dada yangu mwambie mumeo  hadithi yako yote ya maisha'' mwingine alimshauri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved