Waakazi wa eneo la Siaya wameonekana kutoridhishwa na mzunguko mpya uliojengwa mjini humo ambao ni wa kwanza kuwahi kuundwa tangu Kenya ijinyakulie uhuru.
Kulingana na wakaazi, waliazimia kujengewa mzunguko wa kifahari ambao utaboresha na kufanya jimbo lao kuvutia.
Wakaazi walisema kuwa hawakujua kilichokuwa kinajengwa katika barabara hiyo kwa kuwa muundo huo ulikuwa umefunikwa kwa mabati wakati wa ujenzi.
Hatimaye, baada ya ujenzi, mradi huo ulifichuliwa na wakaazi kuona kilichokuwa kimefunikwa ila halikuwafurahisha licha ya kusubiria kwa muda mrefu kwa hamu.
Wengi walikejeli mzunguko huo huku wakipiga picha na kutuma kwenye mitandao ya kijamii, wengine wakiashiria kutoridhishwa na taswira ya mradi huo ambao ulitumia mamilioni ya pesa kuunda.
“Inaonekana kama zizi la ngo’mbe.” Hope Evans alisema.
"Inaonekana kama keki iliyokusudiwa kusherehekea kwa kuzaliwa kwa mtoto." Marwa NgoziNyeusi aliandika.
‘’Inakaa kama mlingoti wa bendera wa huko shuleni kwetu’’ alisema Boogie.
Ila kunao ambao walionekana kupendezwa na mzunguko huo na kusema kuwa ni ishara ya kazi bora.
Walipongeza serikali ya kaunti hiyo hilo kwa kazi hiyo bora iliyofanya kwa minajili ya kustawisha eneo la siaya.
"Mji wetu una sura mpya, angalau kitu kizuri cha kuandika kuhusu kaunti ya mashujaa." Mary Atieno alisema
''Mzunguko wa kwanza katika Siaya. Gavana wangu anafanya kazi kwa busara. Watu wangu walikuwa wanaona vitu kama hivyo kwenye Televisheni. Mungu akubariki Bwana James Orengo'' Wachdog alisema
"Tuna bahati huko Siaya.Huku Kisumu polepole ikibadilika na kuwa Ulaya hivyo ndivyo eneo la Siaya inabadirika kuwa jiji kuu la Nairobi," Maxwel Omolo alisema.