logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwana bodaboda alia kuachwa na mpenzi aliyekuwa anampa Ksh 300 kila siku

Mwanamume huyu alisema amekuwa akimtumia mpenzi wake kiasi cha shilingi 300 kila siku kwa ajili ya kumtunza.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri27 October 2022 - 06:47

Muhtasari


• Mwanamume huyu alisema amekuwa akimtumia mpenzi wake kiasi cha shilingi 300 kila siku kwa ajili ya kumtunza.

Mwendesha bodaboda alalamikia kuachwa na mpenzi wake

Mwanamume mmoja na ambaye ni mhudumu wa bodaboda alisikika akilalama kwenye video iliyoenea wakati ambapo mpenzi wake alimwacha.

Mwanamume huyu aliyejawa na ghadhabu nyingi alisema amekuwa akimtumia mpenzi wake kiasi cha shilingi 300 kila siku kwa ajili ya matunzo.

"Nilikuwa nikimpa msichana huyu shilingi 300 kila siku tangu 2019  ila bado anadanganya.' mwanamume huyu alilalamika.

Kwa kusikitisha, Jamaa huyu aligundua kwamba mpenzi wake alikuwa akiona mtu mwingine na hii ilivunja moyo wake vipande vipande. Hakuamini kwamba angesalitiwa licha ya juhudi zake zote.

Mwendesha bodaboda alisema hakuwahi kumshuku mpenzi wake ni mdanganyifu na alimpenda sana kupindukia.

Kulalamika kwa mwanamume huyu kulifanya watumizi wa mitandao kutuma misururu ya jumbe kumkashfu mwanadada huyo na wengine kumpa pole mwanamume huyo.

"Iwapo jamaa huyu aliamua kuhifadhi pesa hizo, sasa angekuwa na zaidi shilingi laki 4"  @showdadddy alisema..

''Angalau pia yeye aliponda raha na mwanamke huyo mara nyingi miaka hiyo'' @segunbenson40 alisema.

 "Jumla ya pesa anazompa msichana kutoka 2019 hadi 2022 inapaswa kuwa shilingi laki 2. Wasichana wengine ni wabaya naapa." @pelyzon aliapa.

"Sielewi kwa nini msichana hakukupenda na kuendelea kuchukua pesa kutoka kwako!" @tobig014 alishangaa.

"Kwa wakati huo mshahara wa kila mwezi ni bora kuliko pesa za kila siku, labda ungepaswa kumpa pesa kila mwezi."  @tobig014 alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved