"Wahuni sio watu!" Harmonize alalamika baada ya mjakazi wake kupachikwa mimba

Mmoja wa wajakazi wa Harmonize, Chef Rehema, ni mjamzito.

Muhtasari

•Harmonize alimpongeza Rehema kwa ujauzito na kueleza hamu yake kubwa ya kukutana na mtoto anayebeba tumboni.

"Wanaume hawachezi OOO!! Lol, tayari wamefanya hivyo kwa mjakazi wangu. Sasa wamepenyaje VILLAGE?? Jamani wahuni sio watu," alisema

Harmonize (Picha kubwa), Chef Rehema (Picha ndogo)
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Mmoja wa wajakazi wa Harmonize, Chef Rehema, ni mjamzito.

Staa huyo wa Bongo alifichua habari za ujauzito wa Rehema siku ya Alhamisi kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alipakia video ikionyesha tumbo lililochomoza la mpishi huyo wake.

Katika video hiyo, Harmonize anasikika akimwita mpishi huyo wake kuja mahali alipokuwa ametulia na kamera yake. Punde baada ya Rehema  kujitokeza mbele ya Camera, bosi huyo wake anasikika akimpongeza.

"Mbona unajificha Chef Rehema?" Harmonize alimuuliza Rehema kabla ya kutokea.

Baada ya Rehema kujitokeza, bosi huyo wa Kondegang kwa sauti kubwa anasema "Hongera! Chef Rehema Hongera!" 

Katika maelezo ya video, mwimbaji huyo anashangaa jinsi mjakazi huyo wake alivyopachikwa ujauzito.

"Wanaume hawachezi OOO!! Lol, tayari wamefanya hivyo kwa mjakazi wangu. Sasa wamepenyaje VILLAGE?? Jamani wahuni sio watu," aliandika.

Alimpongeza mwanadada huyo kwa ujauzito na kueleza hamu yake kubwa ya kukutana na mtoto anayebeba tumboni.

"Hongera Rehema, Uncle Konde ako hapa akisubiri mwanachama mwingine wa Kondegang," alisema.

Sio mengi yanayojulikana kumhusu mjakazi wa Harmonize, Chef  Rehema na anaonekana kuwa mwanamke mwenye haya.

Takriban miezi mitano iliyopita staa huyo wa Bongo alitoa ahadi ya nyumba na gari kwa mjakazi wake mwingine, Zuwena.

Alichukua hatua hiyo kama ishara ya shukran kwa huduma alizomtolea katika kipindi cha miaka saba ambacho kimepita.

Wakati huo, Konde Boy alitangaza kuwa anapanga kutimiza hadi yake kwa Zuwena kabla ya mwezi huo kuisha.

"Ni kama shangazi yangu. Miaka 7 anajua nakula nini. Ananipikia, ananifulia, ananifanyia usafi, anajua ukichaa wangu wote. Kabla ya Juni namnunulia gari lake la kwanza na kinyumba hata cha chumba 3 mkoani kwao," alitangaza.

Harmonize alifichua kuwa Zuwena ndiye mjakazi wake wa kwanza huku akidai kuwa sio mfanyikazi wake tu bali pia ni kama dada yake.

Alimshukuru sana mwanadada huyo kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akifanya na kumtakia baraka za Maulana.

"Mungu akubariki dada Zuuh maana si kwa vipipi vya sigara ambavyo unavifagia kila siku kwenye mashuka majivu vipi," Alisema.

Harmonize anajulikana kuwatambua na kuwazawadi watu wake wa karibu baada ya kupiga hatua muhimu.