"Nilikuwa na moja tu" - Mulamwah amjibu mwanadada aliyetaka mimba yake

Wengi walihisi mchekeshaji huyo alikuwa akimaanisha mtoto wake mmoja ambaye walibarikiwa na Carrol Muthoni.

Muhtasari

• Mulamwah na mzazi mweziwe muigizaji Sonnie Muthoni walitengana mwezi Oktoba mwaka jana.

Mulamwah amjibu shabiki aliyetaka mimba yake
Mulamwah amjibu shabiki aliyetaka mimba yake
Image: Instagram

Muigizaji na mcheshi Kendrick Mulamwah kwa mara nyingine tena ameibua gumzo lingine linalohusisha familia yake ya mtoto Keilah na mzazi mweziwe Carrol Sonie.

 Mchekeshaji huyo anasema kuwa huenda ile mimba iliyosababisha kuzaliwa kwa mtoto Keilah ndio pekee aliyokuwa nayo na kuwa hana nyingine tena.

Alisema haya alipokuwa anamjibu mtumizi wa mtandao wa Facebook aliyemuomba kumpa mimba ambapo alimjibu kuwa alikuwa na mimba moja tu.

Mtumizi huyo alimtaka Mulamwah kumpa mimba na kutoweka kabisa ila mchekeshaji huyo kwa utani akajibu kwa maneno machache akisema kwamba ile ya Keilah ndio tu alikuwa nayo na kwa sasa hana mimba nyingine ya kupeana tena.

“Mulamwah si unipe mimba halafu upotee,” Mtumizi huyo kwa jina Ann Kangethe alimuomba.

“Nilikuwa tu na moja,” Mulamwah alijibu.

Mulamwah na mzazi mweziwe muigizaji Sonnie Muthoni walitengana mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa miaka michache.

Wawili hao walibarikiwa na mtoto mmoja wa kike kwa jina Keilah ambaye baada ya kuachana kwao alijipata katikati ya tafrani hiyo, huku baadhi wakizua gumzo kuwa huenda ndiye chanzo cha kutengana kwao.

Mulamwah alienda mbele hata zaidi alipoandika ujumbe wenye ukakasi mtanange kwenye mitandao yake akidai kuwa mtoto huyo si wake na kusema mamake alikuwa amejaribu kumuavya, jambo ambalo Sonnie alipinga vikali na kusema kwamba Mulamwah alikuwa anajaribu juu chini ili kumchafulia jina na kumfanya kuonekana mbaya.