Jovial aahirisha kutoa kibao kipya baada ya kuugua

Kulingana na msanii huyo, alikuwa anatarajia kutoa kibao wiki hii, lakini hataweza kwani hayuko kwenye hali ya kutoa kibao.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alifichua kwamba kama timu yake haingekuwa naye hajui mahali angekuwa

Msanii Jovial atachukua muda wa mapumziko kutoka kwa mitandao ya kijamii baada ya kuanguka.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alifichua kwamba kama timu yake haingekuwa naye hajui mahali angekuwa.

Kulingana na msanii huyo, alikuwa anatarajia kutoa kibao wiki hii, lakini hataweza kwani hayuko kwenye hali ya kutoa kibao.

Jovial ana sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yake.

"Mwili yangu imekataa leo ile kuanguka nimeanguka kama ningekuwa  pekeyangu sijui ingekuwa aje, jana nilikuwa naambia timu yangu kimchezo kwwamba sihisi vizuri lakini nitakuwa sawa

Hivi ndivyo watu hufariki, leo wako sawa na kesho wameenda,niruhusu nipumzike nilikuwa niachie kibao kipya lakini nitaihirisha mpaka wiki ijayo,ikiwezekana nitaweza aachia vibao mara mbili

Sitakuwa kwenye mitandao ya kijamii,"Aliandika Jovial.