Kutana na babu ya Zari anayefanana naye kama shilingi kwa ya pili (+picha)

"Nimeipata kutoka kwa babu yangu," Zari alisema.

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto watano alichapisha picha yake moja na ya babu yake kwa ajili ya wanamitandao kulinganisha kufanana kwao.

•Hakuna maelezo mengi yaliyowekwa hadharani kuwahusu babu na nyanya wa mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz.

Mwanasoshalaiti Zari Hassan na marehemu babu yake.
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Siku ya Alhamisi asubuhi mwanasoshalaiti na mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan alionyesha picha ya marehemu babu yake.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa watoto watano alichapisha picha yake moja na ya babu yake kwa ajili ya wanamitandao kulinganisha kufanana kwao.

"Nimeipata kutoka kwa babu yangu," aliandika chini ya picha hizo.

Picha ya babu ya Zari ambayo alichapisha ni ya rangi nyeusi na nyeupe lakini sifa nyingi za nyuso zao zinazofanana zinaweza kutambulika kwa urahisi..

Watumizi wa Instagram waliweza kutambua masikio yao marefu yanayofanana, pua sawa, umbo la midomo yao unaofanana na mwonekano sawa wa nyuso zao.  Wengi walishangazwa na ufanano mkubwa kati ya wawili hao.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za wanamitandao:

@fauzia_assan: Ni pacha wako

@zejest_: Ni hayo masikio marefu ndo umetoa kwa babu yako

@rehemamaminya36: Hahaa, babu sio pua, sio kwa hilo sikio, bora hujachukua zote

@itoluchi30: Kutoka kwenye shingo hadi kichwani, hapana.

@drealkentucky231: Kweli, ukweli usemwe.

@almarula: Jeni zinashangaza!!

Zaidi ya kubainisha kufanana kati yake na babu yake, baadhi ya wanamitandao walithamini na kusifia urembo wa kuvutia wa mwanasoshalaiti huyo.

Zari Hassan alizaliwa na kulelewa nchini Uganda na wazazi wake Waganda Bw Nahur Hassan na marehemu Bi Halima Hassan. Hakuna maelezo mengi yaliyowekwa hadharani kuwahusu babu na nyanya wa mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz.

Mama ya mwanasoshalaiti huyo alifariki mwaka wa 2017, wiki kadhaa tu baada ya kumpoteza aliyekuwa mume wake, Ivan Semwanga.