Soma ujumbe mtamu wa Bobi Wine kutoka kwa mkewe

Wine anafahamika sana kuwa mpinzani mkuu wa serikali ya uganda.

Muhtasari
  • Wawili hao ambao wanachukuliwa kuwa miongoni mwa wanandoa wenye nguvu zaidi nchini Uganda wameoana kwa takriban miaka 11 sasa na wana watoto wanne
Kionozi wa Uganda Bobi Wine kuandaa tamasha la kuchangisha pesa kuwaokoa waganda waliokwama Uarabuni
Kionozi wa Uganda Bobi Wine kuandaa tamasha la kuchangisha pesa kuwaokoa waganda waliokwama Uarabuni
Image: Facebook

Robert Kyagulanyi anayejulikana kwa jina lake la kisanii Bobi Wine, ni mwanasiasa, mwimbaji na mwigizaji wa Uganda.

Yeye ni Mbunge wa zamani wa eneo bunge la Kaunti ya Kyadondo Mashariki katika Wilaya ya Wakiso, katika Mkoa wa Kati nchini Uganda.

Wawili hao ambao wanachukuliwa kuwa miongoni mwa wanandoa wenye nguvu zaidi nchini Uganda wameoana kwa takriban miaka 11 sasa na wana watoto wanne.

Mnamo tarehe 11 Novemba, mke wa Bobi Wine Barbie kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook alipakia picha ya mumewe ikiwa na nukuu ya ujumbe mtamu ambao ulilingana na chapisho lake akisema

"Tazama huyu Binadamu wa ajabu?Yeye ni zaidi ya inavyoonekana.Usingemaliza uwezo wake.Brah, imekuwa zaidi ya miaka Ishirini ya hekima inayotiririka kwangu!Ninakuheshimu sana Taata.Asante kwa masomo ya maisha ya kila siku.Uganda umebarikiwa kuwa na wewe kuwatumikia watu wake katika hatua hii ya maisha yako,"Aliandika mkewe Bobi Wine.

Wine anafahamika sana kuwa mpinzani mkuu wa serikali ya uganda.