"Hadi mtoto wa kike wanamuonea gere!" Kajala awachana machawa Mwijaku, H-Baba, Baba Levo

Kajala amesema kuna machawa wengi Bongo ambao hawana aibu kuwaonea wivu wanawake.

Muhtasari

•Baba Levo, Mwijaku na H-baba wameongoza katika kuibua tuhuma nzito dhidi ya wapenzi hao wawili na baadhi ya wanafamilia wao.

•Kajala amesema  kuwa wapo machawa wengi Bongo ambao hawana aibu hata kuwaonea wivu wanawake.

Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Muigizaji Kajala Masanja amevunja ukimya na kuwajibu machawa wa Bongo ambao wameibua tuhuma nzito dhidi yake na mchumba wake Harmonize.

Chawa maarufu wa Diamond Platnumz Baba Levo na machawa wa zamani wa Harmonize, Mwijaku na H-baba wameongoza katika kuibua tuhuma dhidi ya wapenzi hao wawili na baadhi ya wanafamilia wao.

Katika jibu lake, Kajala amesema  kuwa wapo machawa wengi Bongo ambao hawana aibu hata kuwaonea wivu wanawake.

"Huko kwetu machawa wapo, tena wakikung'ata wanakutoa vipele!!  Sio machawa wa mjini, hadi mtoto wa kike wanamuonea gele!!" mama huyo wa binti mmoja alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya aliyekuwa mwanadani wa Harmonize, Mwijaku kuibua madai kuwa staa huyo wa Bongo alimpa ujauzito Kajala na muigizaji huyo alitaka  kuutoa kwa kuwa haikuwa mapenzi yake kuzaa naye.

Mwijaku ambaye kwa siku za hivi majuzi ameonekana kuwa karibu sana na anayeaminika kuwa hasidi nambari moja wa Harmonize, Diamond aliibua madai hayo baada ya Kajala kuweka video fupi akipokea matibabu hospitalini.

"Tayari dada yetu ameenda kutoa ujauzito, ameona wanapoelekea ni uneconomic freedom kwa familia na yeye anataka pesa," alisema.

Matamshi ya Mwijaku yalizua mjadala mkubwa Bongo ikizingatiwa  kwamba  kwa muda mrefu amekuwa na ukaribu mkubwa na bosi huyo wa Konde Music Wordwide kabla ya kutengana kwao mwezi uliopita.

Wiki jana hata hivyo Harmonize alithibitisha kuwa mchumba wake Kajala anaugua na kumtakia apone haraka.

"Pona haraka mpenzi. Siwezi kusubiri kukuona ukiwa mwenye nguvu tena," staa huyo wa Bongo aliandika chini ya picha ya Kajala akionekana mdhaifu ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwijaku pia aliwahi kuibua madai kuwa Harmonize  anatoka kimapenzi na Kajala  pamoja na bintiye Paula Kajala kwa zamu.

Mwijaku alichukua hatua zaidi na kuenda mpaka kituo cha ustawi wa jamii kumshtaki Harmonize akitaka achukuliwe hatua za kisheria kwa kile alisema kwamba anamdhulumu Paula ambaye ni mtoto.

“Siku moja nilienda kwa Harmonize nikamkuta sebuleni amekaa na Boxer halafu Paula anampapasa kifuani. Mimi kama Mzazi sikupenda, nikamwambia hii sio sawa akaniambia haya ni mambo ya kifamilia yaache, akasema Pesa inaoongea,” alisema.

Siku za nyuma, Baba Levo na H-Baba wamewahi kuonyesha chuki dhidi ya mchumba wa Kajala,  Harmonize na kumtupia cheche za maneno.