'Daktari alisema nimemaliza mayai,'Akothee ajibu madai ya kuwa mjamzito

Kwa haraka sana mashabiki wake walimtumia Akothee jumbe za pongezi.

Muhtasari
  • Alitupilia madai hayo mbali siku ya Ijumaa kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook,hii ni baada ya mashabiki kusema kamba mama huyo wa watoto 5 alikuwa anatarajia mtoto mwingine
'Omondi' na Akothee
Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mjasirimali na msanii shupavu nchini Esther Akoth almaarufu Akothee ametupilia mbali madai kwamba ni mjamzito.

Alitupilia madai hayo mbali siku ya Ijumaa kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook,hii ni baada ya mashabiki kusema kamba mama huyo wa watoto 5 alikuwa anatarajia mtoto mwingine.

Akothee alisema kwamba anatamani kuku na wala sio kwa ajili ana mimba.

Pia aliwatania mashabiki wake na kuwataarifu kwamba daktari alimwambia mayai ya uzazi yamekwisha.

Kwa haraka sana mashabiki wake walimtumia Akothee jumbe za pongezi.

"Kuku wa limau ukiwa na chumvi nyingi😭😭😭😭😭ngoja mimi sio mjamzito, ni utoto inanisumbua. Keep the congratulations haki, mimi hata daktari alisema nimemaliza mayai ,labda miracle baby 🙊,"Aliweka wazi Akothee.