Hakuna mwanaume anayeona 'future' kwa mwanamke mwenye nywele za rangi - Daktari

Kulingana na daktari huyo, mwanamke kupaka nywele rangi moja kwa moja inatuma ujumbe hasi kwa akili za wanaume kuhusu tabia ya mwanamke huyo.

Muhtasari

• Tayari kuna dhana potofu iliyoambatanishwa nayo. Wanaume Wanajua wanachotaka - Dkt Penking alishauri.

Daktari ashauri wanawake kutopaka nywele rangi
Daktari ashauri wanawake kutopaka nywele rangi
Image: Twitter

Daktari mmoja kutoka nchini Nigeria ambaye ni mzungumzaji sana kwenye mitandao ya kijamii amewashauri wanawake wanaotaka ndoa kukoma kufanya baadhi ya mambo ambayo alisema yanawafukuza wanaume ambao wangewafuata na kuwaomba mkono wao katika ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, dakatari huyo anayefaamika kwa jina Doctor Penking aliwashauri wanadada kukoma kupaka rangi kwenye nywele zao kwani hili linawachukiza sana wanaume na kuwaona wanawake hao kama magaidi wasioweza kutulia kwenye ndoa.

Kulingana na daktari huyo, mwanamke kupaka nywele rangi moja kwa moja inatuma ujumbe hasi kwa akili za wanaume na tayari kuna kasumba inayohusishwa na kitendo hicho kuwa mwanamke kama huyo hana mustakabali mwema katika maisha.

“Hakuna mwanamume anayekaribia mwanamke mwenye nywele za rangi (dhahabu, kijani, nk) kwa nia kubwa. Tayari kuna dhana potofu iliyoambatanishwa nayo. Wanajua wanachotaka. Hakuna mwanaume anayeona mustakabali na mwanamke kama huyo,” Dkt Penking alishauri.

Ushauri huo ulionekana kuibua mjadala mkali kwenye mtandao wa Twitter, wengi wakipinga dhana hiyo kwa kusema kuwa wanaume wa siku hizi wanapenda kuona wake zao wakirembeka ikiwemo kupaka nywele zao rangi.

Hata hivyo, pia kulikuweko na wengine waliokubaliana nao huku wakitoa maoni mengine ya kuashiria vitu vingine ambavyo wanaume hawapendi kuona kwa wanawake.

“Hata wanawake walioolewa wanapaka rangi nywele siku hizi, haimaanishi mtu hajashuka, mume wa jirani yangu alimuomba amkate nywele na kupaka rangi iwe nzuri au nyekundu. Ninaipenda lakini siwezi kuifanya sasa kwa sababu ya taaluma yangu,” Paula Ekoja alisema.

“Acha nikushtue mume wangu alinifanya ninyoe nywele zangu na kuzipaka rangi ya dhahabu, nyeupe, kwa kweli rangi yoyote anayojisikia ilinifanya nivae shanga kiunoni ambayo peke yangu siipendi! jisemee na mimi nimejazwa roho sana kweli hayo mambo hata hayaingii kati yangu na Mungu wangu,” Humz Baby alisema.

“Asilimia 60 ya wanawake walioolewa ambao hupaka rangi nywele zao hulala nje ya ndoa zao. Nina takwimu zangu.” NX Alison alitoa takwimu zake.

Maoni yako ni yepi?