Wasanii wa Tanzania tunatumia Muda Mwingi Kushindana na Kupigana Vijembe-Diamond

Aidha msanii huyo alisema kwamba wasanii hao wanapaswa kushindana na wasanii kutoka nchi zingine kama vile Nigeria.

Muhtasari
  • Diamond akizungumza akiwa kwenye harambee msikitini alisema kwamba wasanii wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kupigana vijembe
Diamond Platnumz
Image: Diamond Platnumz Instagram

Naseeb Abdul anayefahamika kwa jina la kisanii Diamond Platnumz na ambaye anafuatiliwa sana kwa ukaribu na mashabiki wake amewasihi wasanii wa Tanzania waache kushandana wenyewe kwa wenyewe.

Diamond akizungumza akiwa kwenye harambee msikitini alisema kwamba wasanii wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kupigana vijembe.

Aidha msanii huyo alisema kwamba wasanii hao wanapaswa kushindana na wasanii kutoka nchi zingine kama vile Nigeria.

"TUACHE KUSHINDANA WENYEWE, TUSHINDANE NA WA-NIGERIA,Wasanii wa Tanzania tunatumia Muda Mwingi Kushindana na Kupigana Vijembe kwa vitu visivyo namsingi, Wakati Wenzetu wa Magharibi (Nigeria) Wanazidi kupiga hatua. Tuache Kushindana Wenyewe," Diamond platnumz alisema.

Pia alisema kwamba uhusiano wake na Mungu uko sawa na imara , kwani watu wamekuwa wakichanganya uimbaji wake na uhusiano wake na Mungu.

Aliongeza kuwa kabla ya kuimba huwa anazungumza na Mungu ili amuongoze kwa njia ipasavyo.