Will Smith asema ‘hasira ya kufungia ndani’ ilimfanya kumpiga kofi Chris Rock katika tuzo za Oscar

Muigizaji huyo amehojiwa kwa mara ya kwanza tangu tukio hilo, ambalo alilitaja kuwa "usiku wa kutisha".

Muhtasari
  • Hapo awali alikuwa amesema mkewe hakumwomba amkabili Rock
  • "Nadhani ningesema ni kwamba huwezi kujua mtu anapitia nini," alisema, bila kufafanua kile alichokuwa akirejelea
  • Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Smith kuhojiwa hadharani kuhusu shambulio hilo
Will Smith akimzaba kofi Chris Rock
Will Smith akimzaba kofi Chris Rock
Image: BBC

Will Smith amesema hasira yake ya ‘kufungia ndani’ ilimpelekea kumpiga kibao mchekeshaji Chris Rock kwenye jukwaa la tuzo za Oscar mwezi Machi.

Muigizaji huyo amehojiwa kwa mara ya kwanza tangu tukio hilo, ambalo alilitaja kuwa "usiku wa kutisha".

Akiwa kwenye kipindi cha The Daily Show akiwa na Trevor Noah, alisema: “Nilikuwa nikipitia jambo fulani usiku huo, unajua?

"Si kwamba hiyo inahalalisha tabia yangu hata kidogo." Smith aliongeza kuwa kulikuwa na "Mambo mengi na matatizo yake", lakini aliongeza: "Mimi tu - nilijisahau."

Smith alivamia jukwaa kwenye hafla ya tuzo ya Hollywood baada ya Rock kufanya mzaha kuhusu kunyolewa kichwa kwa mke wa Smith.Jada Pinkett Smith ana hali ya kupoteza nywele-alopecia.

Hapo awali alikuwa amesema mkewe hakumwomba amkabili Rock.

"Nadhani ningesema ni kwamba huwezi kujua mtu anapitia nini," alisema, bila kufafanua kile alichokuwa akirejelea.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Smith kuhojiwa hadharani kuhusu shambulio hilo.

"Ninaelewa jinsi hiyo ilivyokuwa ya kushangaza kwa watu ... nilikuwa nimeenda. Hiyo ilikuwa hasira ambayo ilikuwa imebanwa kwa muda mrefu sana," alimwambia Noah.

"Huo ulikuwa usiku wa kutisha, kama unavyoweza kufikiria."

Mnamo Julai alichapisha video kwenye YouTube, akijibu maswali ambayo yalionekana kuandikwa na mashabiki kuhusu Tuzo za Academy. Kabla ya hapo, alikuwa ametoa tu taarifa za maandishi kuhusu ugomvi huo.