logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rotimi afunguka kwa nini anataka kupata watoto wengi

Muigizaji huyo alisema kuwa hakutaka kusubiri muda mrefu sana kupata watoto.

image
na Radio Jambo

Habari30 November 2022 - 04:05

Muhtasari


•Rotimi alikiri kwamba kuwa mtoto wa pekee katika familia yao kulimfanya kutaka kuwa na watoto wengi.

•Rotimi aliweka wazi kuwa hataki mwanawe awe peke yake.

Muigizaji na mwanamuziki wa Marekani Olurotimi Akinosho almaarufu Rotimi amefichua sababu kwa nini anataka kuwa na watoto wengi.

Akizungumza kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, Rotimi alikiri kwamba kuwa mtoto wa pekee katika familia yao kulimfanya kutaka kuwa na watoto wengi.

Mume huyo wa malkia wa Bongo Vanessa Mdee aliweka wazi kuwa hataki mwanawe awe peke yake.

Rotimi na Mdee wana mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na wanatarajia mtoto wao wa pili, wa kike.

“Kwa hiyo nataka mwanangu (Seven Adeoluwa Akinosho) awe na mtu ambaye anaweza kumtegemea, ambaye anamuangalia,” alieleza.

"Wanajua watakuwa pale kwa ajili yake. Binti yangu akiangalia upande wake wa kulia, anajua ana kaka mkubwa ambaye anapitia jambo lile lile katika umri huo huo."

Rotimi aliongeza kuwa hakutaka kusubiri muda mrefu sana kupata watoto.

"Unajua sikutaka lile pengo la miaka sita, saba ambapo kimsingi ni watoto tu, kwa hiyo nilitaka wawe karibu sana kiumri na Vanessa alielewa na yeye alitaka jambo hilo hilo. Nilihisi kuwa na mwenza huyo," sema.

Akizungumza katika mahojiano mengine na The Pivot Podcast, Rotimi alisema alitulia kwa mwanamke wa Kiafrika kwa sababu wananyenyekea.

"Unapokuwa na mwanamke wa Kiafrika, unapata mwanamke ambaye ni mwangalifu juu ya kuelewa kwetu kuhusu 'jinsi ya kumtendea mwanaume na jinsi ya kunyenyekea," alisema.

Rotimi alisema Vanessa kando na kuwa mrembo pia anajua jinsi na wakati wa kuwa mgumu.

"Ni uwiano tu ambao ni vigumu kuupata na sisemi kuwa haupati hivyo kwa wanawake wa Marekani lakini wanawake wengi wa Kiafrika wamefanywa kuwa malkia katika akili zao na pia kuwa wake wakuu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved