Mwanaume tafuta hela, mambo ya ku’settle achia vumbi - Willy Lusige, mwanahabari

Ushauri huu wa utani unakuja wakati ambapo mitandaoni kuna mjadala mkali kuhusu ni umri upi sahihi kwa mtu kuanzisha familia.

Muhtasari

• Ushauri huu wa utani unakuja wakati ambapo mitandaoni kuna mjadala mkali kuhusu ni umri upi sahihi kwa mtu kuanzisha familia.

Mwandishi wa habari Willy Lusige
Mwandishi wa habari Willy Lusige
Image: Facebook

Mwandishi wa habari katika kituo kimoja cha runinga humu nchini Willy Lusige amezua utani kwenye mtandao wa Facebook baada ya kutoa ushauri wa utani kwa wanaume.

Lusige aliwashauri wanaume kuwa ukitaka kuwa mwanaume wa kuonewa fahari katika jamii, basi jitume na kujitutumua katika kusaka shilingi kwani heshima haiji bure bila kuwa na pochi nene.

Lusige aliwaambia wale wanaotaka kutulia katika uhusiano au ndoa kabla ya kujitosheleza kifehda kuwa hiyo njia siyo kwani mambo ya kutulia yanafaa yaachiwe tu kwa vumbi.

“Mwanaume tafuta hela, mambo ya ku’settle achia vumbi,” Lusige aliandika huku akimalizia na emoji za kucheka.

Ushauri huu wa utani unakuja wakati ambapo mitandaoni kuna mjadala mkali kuhusu ni umri upi sahihi kwa mtoto wa kiume na yule wa kike kuamua kutulia na kuanza kujenga familia yao.

Baadhi wanahoji kuwa umri sahihi wa mtoto wa kiume ni miaka 30 huku wengine wakipinga kuwa umri si kigezo kamili bali ni kuwa na uwezo wa kifedha kujikimu kwa mahitaji yako yote kabla ya kuongeza familia yenye pia itakuwa inakuangalia kumudu mahitaji yao.

Kwa wale ambao hawajui Lusige, aligonga vichwa vya habari miezi  kadhaa iliyopita baada ya kukorofishana na mtu mmoja aliyejaribu kuingia mbele yake kuongea kwa kamera wakati Lusige alikuwa anaripoti moja kwa moja runingani.

“Baada ya kutembelea Busia katika mkutano wa Azimio la Umoja…” Lusige alikuwa ameanza kabla ya kitendo hicho kutokea.