"Sipendi brown skins!" Mammito afunguka kwa nini anapendelea wanaume weusi

Mamitto alidai kuwa hakupatikana kuhudhuria tamasha la Butita.

Muhtasari

•Lengo la mchezo huo, kulingana na Dkt Ofweneke lilikuwa kujua mpenzi huyo wa zamani wa Butita anapendelea mwanaume mwenye sifa zipi.

•Mamitto pia alihitajika kuchagua kati ya wanamuziki Khaligraph Jones na Willy Paul ambapo alimchagua Jones.

mammito
Mchekeshaji Eunice Mammito mammito
Image: HISANI

Siku ya Jumanne jioni, mchekeshaji Eunice Mamitto alikuwa mgeni katika shoo ya Dr Ofweneke kwenye stesheni ya TV47.

Katika shoo hiyo, mchekeshaji huyo alishirikishwa katika mchezo wa kuburudisha ambapo alitakiwa kuchagua kati ya wasanii wawili aliopewa. Lengo la mchezo huo, kulingana na Dkt Ofweneke lilikuwa kujua mpenzi huyo wa zamani wa Butita anapendelea mwanaume mwenye sifa zipi.

Katika kitengo cha kwanza, Mamitto alitakiwa kuchagua kati ya waigizaji maarufu Kagwe Mungai na Luwi Capello.

"Nachagua Kagwe. Sipendi brown skins," alisema.

Huku akitetea chaguo lake, mchekeshaji huyo aliibua mambo kadhaa aliyohusisha na wanaume wenye ngozi za kahawia.

"Wanalia, tena vipondozi, tena mascara! unaamka asubuhi tena sijui afanye nini. Wamezidi sana. Utapata anapaka nyusi rangi asubuhi," alisema.

Katika kitengo cha pili, mchekeshaji huyo alihitajika kuchagua kati ya mtangazaji Mark Masai na mwanamitindo Sean Andrew.

Bila kusita, Mamitto alimchagua mjukuu huyo wa Kibaki.

"Nikiwa na pesa ya Andrew naweza kumweka Masai," alisema.

Mamitto pia alihitajika kuchagua kati ya wanamuziki Khaligraph Jones na Willy Paul ambapo alimchagua Jones.

"Khaligraph bila shaka. Usalama mazee, huyu ni mtu ati nitaanza kusumbuana nikiwa naye 'nitapigia mpenzi wangu,'.. Willy ako na masuala. Anapitia mambo mengi," alisema mchekeshaji huyo.

Mchekeshaji huyo aliweka wazi kuwa hakuhudhuria tamasha la mpenzi wake wa zamani Butita ambalo lilifanyika hivi majuzi katika ukumbi wa Kenya Cinema. Alidai kuwa hakupatikana kuhudhuria wakati huo.

 Terence Creative na Milly Chebby, The Wajesus Family, King Kaka na Nana Owiti, Mulamwah, Abel Mutua, Phil Karanja na Njugush ni miongoni mwa wasanii ambao walijitokeza kumsapoti mchekeshaji huyo.