logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wema Sepetu amlilia Mungu amjalie mtoto baada ya kutoweza kuzaa kwa miaka mingi

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alimuomba Mungu amjalie mtoto siku moja.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku02 December 2022 - 10:03

Muhtasari


•Wema aliandika ujumbe huo chini ya picha yake akiwa amemshika mtoto mchanga ambayo alipakia kwenye Instagram.

•Wema aliwahi kufunguka kuhusu  tatizo kwenye tumbo lake la uzazi linalomzuia kushika ujauzito

Muigizaji mashuhuri wa filamu za Bongo Wema Sepetu ameendelea kueleza hamu yake ya kupata mtoto wa kwake.

Katika chapisho lake la hivi punde, mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alimuomba Maulana amjalie mtoto siku moja.

Aliandika ujumbe huo chini ya picha yake akiwa amemshika mtoto mchanga ambayo alipakia kwenye Instagram.

"Eh Mungu tafadhali nibariki na wangu siku moja🙏🙏🙏," alisema.

Wema alikiri kuwa kumtazama mtoto huyo mchanga mikononi mwake kulimfanya ajisikie kuwa kuenda naye awe wake.

"Nilitamani nikimbie naye wallahy🥺🥺🥺" alisema.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri waliunga mkono dua la muigizaji huyo na kumuomba Mungu amtimizie.

officialnandy : ❤❤❤🙏

dullamakabila: Utapata Inshallah @wemasepetu

auntyezekiel: Inshallah

qute_centa Upo kama mimi. Nikiona vichanga natamani niviibe nikimbie navyo ❤❤❤ wakati wetu upoo😍

tuongeeuzazi Siku yaja, Mungu atakushangaza

Hadi wa leo, Wema Sepetu ambaye ana umri wa miaka 32 bado hajaweza kumshika mtoto kutoka tumboni mwake.

Kwa miaka mingi, muigazaji huyo amekuwa akishambuliwa na kukejeliwa mitandaoni kutokana na hali yake. Wengine hata hivyo wamekuwa wakimfariji na kumtia moyo mpenzi huyo wa zamani wa Diamond.

Takriban miaka minne iliyopita Wema aliwahi kufunguka kuhusu  tatizo kwenye tumbo lake la uzazi linalomzuia kushika ujauzito.

“Unajua mimi nilikuwa na tatizo kubwa sana kwa upande wa tumbo langu la uzazi lililosababisha nisiweze kuzaa kwa muda wote huu. Ngoja niweke wazi leo watu wajue, mimi nina ugonjwa ambao unasababisha mayai yangu ya uzazi kutoboka na kushindwa kupevusha mbegu za uzazi," Alisema katika mahojiano na Global Publishers.

Licha ya kuwa na tatizo kwenye tumbo la uzazi, muigizaji huyo mwenye sauti nzuri kweli amekuwa akionyesha wazi kuwa bado hajapoteza matumaini ya kuwahi kukumbatia mtoto wake kuzaa katika siku za usoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved