Seneta Mteule Karen Nyamu amemaliza uhusiano wake na msanii wa Mugithi Samidoh baada ya Ksaren na mkewe Samidoh kuvuma sana mitandaoni siku ya Jumamosi.
KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram Nyamu alisema alichukua uamuzi wa kusitisha uhusiano wake na babake mtoto na sasa ex.
"Wanawake wakuu na wenye nguvu watathibitisha kwamba mara nyingi kiungo chetu dhaifu ni wanaume tunaojihusisha nao. Ninaacha mtindo huo," alisema.
"Nimefanya uamuzi makini wa kukomesha uhusiano wangu na baba wa watoto wangu na sasa ni wa zamani."
Nyamu aliandika zaidi kuwa hakuwa na majuto kutokana na kile kilichotokea Dubai, na kuahidi kuwa tukio hilo lilikuwa la mwisho.
"Sitamani ningefanya mambo kwa njia tofauti," Nyamu alisema.
"Najua nilipaswa kumpigia simu na kumaliza kimya kimya, lakini niliamua kuweka hadharani kama drama na utata ulivyo," alisema.
Machapisho yake yanakuja saa chache baada ya drama kushuhudiwa siku ya Ijumaa usiku kati ya mke wa Samidoh naye huko Dubai.
Ilianza wakati Nyamu alienda moja kwa moja hadi pale ambapo Samidoh alikuwa ameketi na kukaa kwa nguvu kwenye mapaja yake.
Edday, alisimama na kumshika mkono mumewe hata wale wanausalama walipojaribu kuwatenganisha wanawake hao wawili.