Harmonize ajibu madai ya kumcheza kajala na video Vixen wake

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Tanzania, Sophie hata hivyo alikanusha kuwa na uhusiano wowote na nyota huyo

Muhtasari
  • Hata hivyo alisema anafurahi kuwa Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Fridah Kajala wameachana na kumuomba Harmonize kutafuta msichana wa aina yake
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Mwimbaji kutoka Tanzania Harmonize amekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na video vixen wa video yake ya ‘Amelowa’.

Harmonize aliyekasirika alimkashifu vikali mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Sophie akisema hawajawahi kukutana baada ya kurekodi video.

Mkali huyo wa 'Uno' alimtaja vixen kuwa mtu asiye na shukrani ambaye hakuthamini nafasi aliyompa ili kutimiza ndoto zake.

“Sijui wewe!! Acha kumzungumzia kaka yako aliyesaidia kutimiza ndoto zako, niheshimu.

Hujawahi kuniona baada ya video, hili ndilo tatizo la kuwa mnyenyekevu, unawapa watu fursa na wanafikiri ni sawa na wewe,” aliandika Harmonize kwenye stori zake za Instagram.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Tanzania, Sophie hata hivyo alikanusha kuwa na uhusiano wowote na nyota huyo akisema uvumi huo pia ulimpata bila kufahamu.

Hata hivyo alisema anafurahi kuwa Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Fridah Kajala wameachana na kumuomba Harmonize kutafuta msichana wa aina yake.

“Mara ya mwisho kuongea na Harmonize ni wakati wa kushoot video, hatujawasiliana tangu wakati huo, amekuwa bize na mambo yake na mimi nimekuwa bize na zangu.

"Hata hivyo nilifurahi kwamba aliachana na Kajala na sijali kuchukua nafasi yake ikiwa Harmonize anataka hivyo," Sophie alisema.