logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchungaji amwaga mafuta ya upako kwenye viti, awataka watu kulipa 3K kukalia ili kupata muujiza

Kila muumini alitakiwa kulippa 3k kukalia kiti chenye upako kwa saa 2 pekee.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku31 December 2022 - 07:29

Muhtasari


• Kila muumini alitakiwa kulippa 3k kukalia kiti chenye upako kwa saa 2 pekee.

• Washiriki waliambiwa kuwa wakitoa 3K na kukalia kiti mwisho wa mwezi wangepata 37K.

Mchungaji akitakasa viti vya kanisani,

Picha za kushangaza kutoka nchini Zimbabwe zikimuonesha mtu anayetajwa kuwa mchungaji wa kanisa moja alivipaka viti maalum vya kanisani mafuta ya upako zimezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Kulingana na taarifa kutoka blogu za nchini humo, mchungaji huyo alikuwa anawaambia waumini kuwa viti hivyo anapovitakasa kwa mafuta ya upako vinakuwa vitakatifu na vyenye nguvu za kipekee.

Kufuatia hilo, aliwataka yeyote aliyekuwa na haja ya kupata muujiza wa kufunga mwaka kukalia kiti hicho baada ya kulipa pesa taslimu shilingi elfu tatu na mia saba za benki kuu ya Kenya ambazo ni sawa na Dola 30 za Kimarekani ili kukalia kiti hicho kwa saa mbili tu!

Kulingana na maelezo hayo, washiriki wa kanisa hilo wanaaminishwa kwamba pindi watakapolipa USD 30 kwa ajili ya kiti, watakuwa na USD 300 au zaidi kwa muujiza katika mwezi mmoja.

Kando na kutokwa jasho ili kutoka kima hicho kikubwa kwa ajili ya muujiza wa kitita kirefu cha pesa mwisho wa mwezi, waumini wale ambao watalipia kiti hicho watakuwa na unyevunyevu katika makalio yao katika muda wote wa ibada, kwani mchungaji huyo alionekana akimimina mafuta mengi ya upako na si kunyunyiza tu.

Katika miaka ya hivi karibuni, watu wengi katika bara la Afrika wamekuwa wakiibua maswali mengi kuliko majibu kuhusu uhalali wa Watumishi wa Mungu ambao wamekuwa wakifanya kanisa kuwa majumba ya utumwa kwa kuwaaminisha waumini mambo mengine ambayo katika nadharia hayawezi kutokea pasi na mtu kujituma – mfano mtu kuombewa ili kupata pesa zimerundikwa kwenye akaunti yake bila kufanya kazi!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved