Je, Harmonize alichukua gari alilomnunulia Kajala? - ukweli hatimaye wafichuka

Gari hilo jeusi bado lilikuwa na namba za usajili 'KAJALA'.

Muhtasari

•Muigizaji huyo alionekana akiendesha gari hilo aina ya Range Rover wakati akienda kumsurprise binti yake Paula Paul.

•Harmonize alimnunulia Kajala gari aina ya range rover mapema mwaka jana wakati alipokuwa akiomba msamaha .

Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Inaonekana kwamba staa wa Bongo Harmonize hakuchukua gari alilompa aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja kama ilivyodaiwa hapo awali.

Siku ya Jumamosi, muigizaji huyo alionekana akiendesha gari hilo aina ya Range Rover wakati akienda kumsurprise binti yake Paula Paul. Gari hilo jeusi bado lilikuwa na namba za usajili 'KAJALA'  kama ilivyowekana  Harmonize.

Kajala alimbeba binti huyo wake wa pekee kwa gari hilo hadi eneo ambapo alikuwa amepanga kumkabidhi zawadi ya gari aina ya CROWN ambalo alimnunulia. Alisema alimnunulia Paula zawadi hiyo maalum ili kuokoa nauli ya teksi.

"Usilie, bajeti ya Uber," Kajala alisikika akimwambia Paula huku akimtuliza baada kushindwa kuuzuia furaha yake na kuangua kilio cha furaha punde alipofumbua macho na kuona kile ambacho mama yake alikuwa amemfanyia.

"Asante mama, nakupenda sana," Paula alisema.

Mpenzi huyo wa zamani wa Harmonize pia alizidiwa na hisia baada ya kuona jinsi binti yake alivyoipenda zawadi aliyomnunulia.

Wiki chache zilizopita tetesi kuwa Harmonize alichukua gari na vitu vingine alivyokuwa amemnunulia muigizaji huyo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Alidaiwa kuchukua hatua hiyo baada ya uhusiano wao kugonga ukuta.

Kajala alionekana akiendesha gari ambalo alinunuliwa na Harmonize
Image: INSTAGRAM// PAULA KAJALA

Baadaye hata hivyo, mama huyo wa mtoto mmoja alionekana akiwa kwenye gari hilo alilopatiwa kama zawadi wakati akitembelea duka la bintiye.

Mwandani wa zamani wa Harmonize, H-Baba ambaye sasa anafanya kazi na Diamond Platnumz alidai kuwa muigizaji huyo aliondoka na vitu vyote ambavyo bosi huyo wa Konde Music Worldwide alimnunulia na kumuacha hohehahe.

Wiki kadhaa zilizopita, machawa maarufu Baba Levo na Mwijaku walimjia juu Kajala na bintiye Paula kwa kile walichosema kuwa wawili hao walimfyonza kavu Harmonize na baadaye kumtoroka mwishoni mwa siku.

Mwijaku ambaye amekuwa na ukaribu mkubwa na Harmonize kwa muda mrefu alimwagiza muigizaj huyo arejeshe gari alilopewa.

“Hapana, arudishe magari ya watu ndio nimuombe radhi. Rudisha magari kwanza ndio nikuombe radhi. Cha kwanza nimekuta meseji DM, akani’unfollow na kisha kuniblock. Yale magari arudishe,” Mwijaku alisema katika mazungumzo na Levo.

Harmonize alimnunulia Kajala gari aina ya range rover mapema mwaka jana wakati alipokuwa akiomba msamaha na kutia juhudi kubwa kufufua mahusiano yao ambayo yalikuwa yamekufa mwezi Aprili 2021.