Pastor Ng'ang'a kumsaidia Kanyari kupata mke katika kanisa lake

Kanyari alisema Ng’ang’a anamtaka kutulia na ameamua kumtafutia mke.

Muhtasari

•Kanyari amekuwa single kwa zaidi ya miaka mitano baada ya kuachwa na mwimbaji wa nyimbo za injili Betty Bayo.

•"Mchungaji Ng'ang'a anasisitiza nioe lakini sijatulia kuoa. Anataka kusimamia harusi yangu."

Ng'ang'a amshauri Kanyari aoe tena
Ng'ang'a amshauri Kanyari aoe tena
Image: Maktaba

Mwanzilishi wa kanisa la Neno Evangelism Mchungaji James Ng'ang'a anatafuta mwanamke wa kuolewa na mchungaji mwenzake Victor Kanyari.

Kanyari amekuwa single kwa zaidi ya miaka mitano baada ya kuachwa na mwimbaji wa nyimbo za injili Betty Bayo.

Akizungumza na mwandishi Elizabeth Ngigi, Kanyari alisema Ng’ang’a anamtaka kutulia na ameamua kumtafutia mke.

“Bado sijaolewa kwa vile sijawa makini na suala hilo, nikipata mke nitafunguka sana kuhusu suala hilo,” alisema.

Kanyari alisema Ng'ang'a amemwalika katika kanisa lake kwa vile kuna wanawake wengi wasio na waume.

"Mchungaji Ng'ang'a anasisitiza nioe lakini sijatulia kuoa. Anataka kusimamia harusi yangu."

Kanyari alisema hayuko tayari kuanza kupata watoto bado.

"Hakuna kitu kikubwa kinachonizuia kuolewa lakini kupata tena wale watoto wadogo sio kazi rahisi. Nitaipata nikiwa tayari," alisema.

Kanyari ambaye ana watoto wawili na mke wa zamani Bayo alisema alitaka kupata watoto sita.

“Nikipata mwanamke ambaye atazaa watoto wanne kwa muda mfupi, litakuwa jambo jema,” alisema.

Mwezi Oktoba 2022, Kanyari alisema hana haraka ya kuchumbiana na mtu lakini yuko tayari kuunganishwa na mwanamke 'mzuri' anayevutiwa.

"Mimi bado sijaoa sana, Sijapata mtu nitafurahi Mpasho wakinitafutia msichana mzuri wa kuoa, wapo wanawake wazuri lakini sijaamua ni yupi bado," alisema.

Alipotakiwa kueleza sifa anazotafuta kwa mwanamke, Mchungaji Kanyari alisema haangalii mwonekano bali atamwomba Mungu amuongoze katika kuchagua.

Utafsiri: Samuel Maina