Juma Jux aonekana na 'pacha' wa Vanessa Mdee kwenye ndege moja

Mwimbaji huyo pia alionyesha nyakati za kimapenzi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Muhtasari

•Jux alionekana akifurahia muda na mwanadada ambaye anafahamika kuwa Karen Bujulu, ambaye alichumbiana naye mwaka jana, na alikuwa video vixen wake.

•Wawili hao walikuwa wanaelekea Paris, mahali Juma Jux anapopenda kuenda likizo. 

Juma Jux na Karen kwenye ndege moja
Image: INSTAGRAM

Juma Jux ameonekana akiwa na mwanamke anayefanana sana na aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee.

Katika video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kumuona Jux akifurahia muda na mwanadada ambaye anafahamika kuwa Karen Bujulu, ambaye alichumbiana naye mwaka jana, na alikuwa video vixen wake.

Mwimbaji huyo pia alionyesha nyakati za kimapenzi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa upande wake Karen alinukuu picha ya ndege, "Wakati huu ninashika hisia na safari za ndege."

Wawili hao walikuwa wanaelekea Paris, mahali Juma Jux anapopenda kuenda likizo. Hata mashabiki wao walifurahi kwamba wawili hao wamerudi pamoja. Soma baadhi ya maoni hayo hapa chini;

tontofloxy...Msalimie jumaaa

dorice_8four..Mama Jux ingia paris

salazahke...Si ndio juma jux huyu hapa

lynee_mtandi...Kumbe upo na juma napenda couple yenu 😍😍

Katika video zilizofuata, Juma Jux alionesha amefika Ufaransa, huku akimuonyesha rafiki yake na eneo walilokuwa.

Pia walishiriki chakula cha jioni na tuliweza kuona kuna marafiki wengine, lakini hakugeuza kamera upande huo. Alionyesha tu rafiki wa kiume akiwa na chakula chake cha jioni cha kifahari.

Juma na Karen walivuma mitandaoni mwaka wa 2022 alipomtambulisha kama mwenza wake mnamo siku ya wapendanao, baadae iligeuka kuwa wimbo. Pia walienda likizo pamoja.

Karen ni mwanamke wa Kitanzania Mnyarwanda ambaye anapenda kusafiri na ana maudhui ya mazoezi ya mwili.

Jux basi wakati fulani aliacha ghafla kusambaza maudhui yake kwenye majukwaa yake, na kutuma ishara kuwa imekwisha. Muda mfupi baadaye, Huddah Monroe alianza kuonekana naye.