'Wanaoeneza uvumi wa D poleni,'Mama Trio Mio ajibu madai ya msanii huyo kupata D

Hata hivyo mama huyo hakufichua alichojizolea msanii huyo huku akisema kwamba anajivunia, matokeo ya mwanawe.

Muhtasari
  • Katika taarifa yake iliyoandikwa Ijumaa, Januari 20, Irma Sofia alieleza kuwa wengi wangesikitishwa na uvumi huo kuhusu mwanawe
Trio Mio
Image: Instagram

Mamake msanii maarufu Trio Mio amekanusha madai kwamba mwanawe alipata D katika matokeo ya hivi punde ya 2022 yaKCSE.

Katika taarifa yake iliyoandikwa Ijumaa, Januari 20, Irma Sofia alieleza kuwa wengi wangesikitishwa na uvumi huo kuhusu mwanawe.

Alisema msanii huyo mashuhuri alifaulu katika mtihani huo uliotangazwa na Waziri Ezekiel Machogu.

Hata hivyo mama huyo hakufichua alichojizolea msanii huyo huku akisema kwamba anajivunia, matokeo ya mwanawe.

"Sitapumua kwa sababu matokeo ya KCSE yametangazwa? Tulia.

"Mvulana alifanya bora yake na ninajivunia sana. Na wale wanaobashiri D. Samahani!" soma taarifa hiyo kwa sehemu.

Kwa hiyo, baada ya kutoa taarifa hiyo msanii huyo aliweka sawa kwenye mitandao yake ya kijamii.

Sofia alikuwa akijibu baada ya madai kuwa msanii huyoalipata alama ya D kuibuka kwenye mitandao ya kijamii.

Ripoti hizo zilishuhudia msanii huyo akivuma kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya Wakenya pia wakwazima waliokuwa wakimkejeli msanii huyo.