"Mtoto bwatata!" - Kutana na kipenzi kipya cha rapa Stivo Simple Boy (+video)

Katika video hiyo, mwanadada huyo alijitambulisha kama mpenzi wa Simple Boy.

Muhtasari

• Katika video hiyo, mwanadada huyo alisikika akiwasihi wanamitandao kufuatilia akaunti mpya ya Simple Boy.

•Pritty Vishy alimshutumu mpenzi huyo wake wa zamani kwa kutafuta kiki kwa kutumia mwanadada huyo.

Mwanamuziki Stivo Simple Boy ametambulisha mpenzi mpya
Image: INSTAGRAM

Rapa mashuhuri kutokea Kibra, Stephen Otieno Adera almaarufu Stivo Simple Boy, anadaiwa kupata mpenzi mpya, takriban mwaka mmoja baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu Pritty Vishy.

Siku ya Jumamosi, msanii huyo alichapisha video ikimuonyesha akiwa ametulia na mwanamke mrembo anayejitambulisha kama @m.arianah_ kwenye Instagram ambaye alijitambulisha kama mpenzi wake.

 Katika video hiyo, mwanadada huyo alisikika akiwasihi wanamitandao kufuatilia akaunti mpya ya Simple Boy.

"Vipi wadau, natumai mko sawa. Nataka msapoti akaunti mpya ya mpenzi wangu kwenye Instagram stivo_simpleboy1, tutashukuru," alisema kabla ya Stivo Simple Boy kumbusu kwenye paji la uso.

Kufuatia hilo, mwanamuziki huyo alimmiminia mpenzi wake maneno matamu ya mahaba na kutoa shukran za dhati kwake kwa sapoti kubwa ambayo alimuonyesha.

"Kichuna mtoto bwatata, rangi chingli chingli nashukuru sana kwa sapoti kipenzi @m.arianah_... Asante kwa sapoti na tour ya Africa Kusini ipo sasa," aliandika chini ya video hiyo.

Mpenzi wake wa zamani, Pritty Vishy ni miongoni mwa wanamitandao wengi waliotoa maoni yao kwenye video hiyo.

Huku akitoa maoni kwenye video iliyochapishwa tena na blogu moja, alionyesha kushangazwa na kile alichokiona.

Pia alimkosoa mpenzi huyo wake wa zamani kwa jinsi alivyombusu mrembo huyo anayedaiwa kuwa mridhi wake.

"Aai, leoo ni kumoto manze, hio mwaah ya ex inakaa aje kwani, adi imechekesha dem yake," alisema.

Baadhi ya wanamitandai walionekana kufurahishwa na jibu lake huku wengine wakidai kuwa aliumia kwa kuwa bado hajasonga mbele na maisha yake.

Akijibu kupitia ukurasa wake, Vishy hata hivyo alikanusha madai ya kuwa bado ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo.

Aliendelea kumshutumu mpenzi huyo wake wa zamani kwa kutafuta kiki kwa kutumia mwanadada huyo

." Nikikuambia au nikuonyeshe jinsi kulivyo uwanjani, nyote mtaacha kuwa na utoto hapa.Ni vile naomboleza sitaki maneno kusema kweli, lakini ikiwa ni kuhusu kusonga mbele, watu wangu, hiyo si ngumu.

Tena mnadanganywa hapa na kiki alafu mnaanza chuki.Tulieni buana mtolewe wimbo muache hasira nyingi," alisema.

Mwaka jana, baada ya mahusiano ya Stivo na Vishy kugonga ukuta, mwanamuziki huyo alidaiwa kuchumbiana na mwanadada mwingine aliyetambulishwa kama Gee ila baadaye ikabainishwa kuwa kiki.