Mke wa mwimbaji Guardian Angel aliwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram.
Katika kipindi hicho wanamitandao walimuuliza maswali mengi kuhusu maisha yake, familia yake, ndoa, kazi na mambo mengine.
Mtumiaji mmoja wa Instagram alitaka kujua ikiwa anaweza kurudiana na mume wake baada ya kukanyaga nje ya ndoa.
"Je, unaweza kurudi kwa mpenzi wako kama alitoka nje ya ndoa," shabiki aliuliza.
Alijibu, "Wow, ndiyo na hapana, lakini itategemea."
Katika kipindi hicho cha Q&A, mama huyo wa watoto watatu wakubwa pia alilazimika kujibu kuhusu iwapo anapanga kupata mtoto pamoja na mume wake Guardian Angel.
Je, Unapanga kupata mimba?" shabiki mmoja alimuuliza.
Musila ambaye alionekana kukerwa na swali aliloulizwa alijibu, "Je, hiyo inaongezaje thamani ya maisha yako??"
Pia alijibu vivyo hivyo wakati mtu mwingine kwa Instagram alipotaka yeye na Guardian walete mtoto wao duniani.
Kwa sasa Bi Musila ana watoto watatu wakubwa, wawili wa kiume na msichana mmoja.
Wakati huo huo, Bi Musila alibainisha kwamba hawezi kuishi bila maji, chakula na mume wake.
Musila ,53, na Guardian Angel ,33, walifunga pingu za maisha mapema mwaka jana baada ya kuchumbiana kwa takriban mwaka mmoja. Wawili hao wamekuwa wakifurahia ndoa yao na kushiriki nyakati nzuri za mahusiano yao kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati huo huo, Bi Musila alibainisha kwamba hawezi kuishi bila maji, chakula na mume wake.
Hivi majuzi, Guardian Angel alimhakikishia mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kwamba hana majuto yoyote kwa kuamua kushiriki maisha naye huku akisema kuwa anaweza kufanya hivyo tena na tena.
"Peter Omwaka, ningeolewa nawe tena," aliandika kwenye picha ya kumbukumbu ya harusi yao inayoonyesha wakiwa wamekumbatiana.
Katika jibu lake kwa mke wake, Guardian Angel alisema, "Kukupenda ni maisha yangu Malkia wangu"
Mwimbaji huyo pia alichapisha picha yake na mkewe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha na emoji za moyo zinazoashiria mapenzi.
"Mpenzi wangu," Musila alijibu chini ya picha hiyo.