logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ni kubaya!Ujumbe wa Diana Marua kuhusu aliko Mueni wazua gumzo

"Tusimshirikishe Yesu palipo na kukosa shukurani, uchungu na chuki. Upendo na Nuru❤"

image
na Radio Jambo

Makala15 February 2023 - 11:37

Muhtasari


  • Diana alijibu huku akisisitiza kuwa mama Mueni hakuwa na shukrani kwa kila kitu walichomfanyia yeye na mtoto wake

Familia ya Bahati ni familia kubwa iliyobarikiwa. Diana na Bahati wana watoto 4 huku ueni akiwa mtoto wa Bahati na aliyekuwa mpenzi wake.

Mwaka jana Mueni alijiunga na Morgan na Heaven katika shule yao mpya, Juja Preparatory School. Mueni angekaa na akina Bahati siku za shule na wikendi aliruhusiwa kwenda kumtembelea mama yake.

Shule zilipofunguliwa mapema mwaka huu Mueni hakuwa amerejea katika himaya ya Bahati wala hakuwepo watoto walipokuwa wakinunuliwa sare za shule na vifaa vya kuandikia.

Aidha chapisho la leo kwenye ukurasa wake wa twitter  Diana Bahati limeibua hisia nyingi kuhusu aliko Mueni.

Diana alichapisha video ikimpeleka Morgan, Heaven na Majesty shuleni ikiwa na nukuu inayosomeka,

"There Goes my Pride and Joy😍 Forever in my heart @morgan_bahati💙 @heavenbahati💖 @majestybahati💙"

Mashabiki wa Diana walitangulia kutoa maoni kuhusu chapisho hilo wakisema wanataka Mueni arudi pamoja na ndugu zake kama walivyokuwa hapo awali. Mmoja aliandika,

"imagine kama Mueni alikuwepo pia😭 Vyovyote ilivyokuwa, nakemea roho ya utengano kwa Jina la Yesu! Amani itawale na Mungu Amrudishe Mtoto Mueni nyumbani kwa ndugu zake😍❤" Darmat

Diana alijibu huku akisisitiza kuwa mama Mueni hakuwa na shukrani kwa kila kitu walichomfanyia yeye na mtoto wake.

"Tusimshirikishe Yesu palipo na kukosa shukurani, uchungu na chuki. Upendo na Nuru❤"

Hata hivyo inadaiwa kuwa ugomvi kati ya Diana na aliyekuwa mpenzi wa Bahati, Yvette Obura ndio ulisababisha Mueni kuacha kuondoka na akina Bahati.

Mwaka jana, mwishoni mwa Septemba, Diana na Yvette waliacha kufuatana kwenye Instagram. Siku chache baada ya kutofuatana, Diana Bahati alitangulia kufuta video ya Youtube aliyoifanya na mama Mueni akionyesha jinsi ustadi wao wa malezi mwenza.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved