Aliyekuwa mpenziwe Mulamwah asema hajawahi jutia kumuacha

Wawili hao waliachana Desemba 2021, huku Carol akifichua kuwa aliachwa na baba wa mtoto wake.

Muhtasari
  • Pia alisema kwamba hajutii makosa yake maishani, akiona yote kama masomo muhimu
Carol Muthoni katika studio za Radio Jambo
Carol Muthoni katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Aliyekuwa mpenzi wa Mulamwah Muthoni Ng'ethe 'Sonie' amezungumza kuhusu kukatisha uhusiano wake na mcheshi huyo, akisema hajawahi kujutia chaguo lake.

Wawili hao waliachana Desemba 2021, huku Carol akifichua kuwa aliachwa na baba wa mtoto wake.

Wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu kwenye Instagram siku ya Jumatatu, shabiki mmoja alimuuliza Sonie: "Je, bado unajuta kumalizia mambo na baba kwa mtoto wako?"

Kwa kujibu, alionekana kushangazwa na swali, akisema: "Bado? Sijawahi kusema ninajuta."

Maoni kutoka kwa Sonie yanakuja huku kukiwa na uvumi kwamba Mulamwah kwa sasa anachumbiana na Ruth K, 'kipenzi' chake.

Sonie ambaye mwezi huu aliteuliwa kuwania tuzo ya Ladies in Media, alieleza kuwa licha ya kuwa mama, pia anapata muda wa kufurahia maisha yake.

Shabiki mwingine alimuuliza Carol ni nini kinachomtia moyo kufanya kazi kwa bidii maishani, naye akajibu:

"Ninaogopa umaskini na ukweli kwamba pesa ni tamu nataka kutafuta kila wakati."

Pia alisema kwamba hajutii makosa yake maishani, akiona yote kama masomo muhimu.