Harmonize kugawanya mali yake na mke wake wa zamani baada ya kushinda kesi ya talaka dhidi yake

Sarah alipakia uujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akimshukuru Mungu kwa ushindi huo.

Muhtasari
  • Taarifa zinaonyesha kuwa nyumba ya sasa anayoishi Harmonize huko Madale inaweza kuwa moja ya nyumba zitakazogawanywa
Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Sarah Michelloti
Image: HISANI

Mwimbaji mahiri wa Tanzania Rajab Abdul Kahali almaarufu kwa jina la kisanii kama Harmonize amepoteza kesi mahakamani dhidi ya mke wake wa zamani.

Msanii huyo wa Bongo Flava alifikishwa mahakamani na aliyekuwa mke wake Sarah baada ya kuachana kwa uchungu na kusababishwa na tetesi kuwa Harmonize alikuwa akimcheza. wa Kwangwaru na pia mahakama iliagiza wawili hao wagawane mali yote ambayo waliipata wawili hao wakiwa pamoja kama mke na mume.

Taarifa zinaonyesha kuwa nyumba ya sasa anayoishi Harmonize huko Madale inaweza kuwa moja ya nyumba zitakazogawanywa.

Sarah alipakia uujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akimshukuru Mungu kwa ushindi huo.

Kulingana na mwanablogu wa Tanzania Juma lokole;

 "SARAH AMESHINDA KESI ALIYOFUNGUA ZIDI YA ALIYEKUWA MUME WAKE ....!! UNAAMBIWA SARAH ALIKUWA ANAFATILIA HI KESI KWA MAPANA ..... KAKA YENU SI ALIMKANA SARAH KUWA HAKUWAHI KUMUOWA πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ..... KUMBE KASAHAU YEYE NDIYE ALIYEMCHUKULIA KIBALI CHA KUISHI NCHINI KAMA MUME WAKE πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ....!! AKAULIZWA SASA UNAKANA UJAMUOWA HUYU SARAH KWAIYO HI KESI TUIPELEKE UHAMIAJI WAKUFUNGULIE WAO KWA ULICHOKIFANYA…? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ KAKA YENU AKAKUBALI APO APO SAWA NILIMUOWA πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚SARAH ANAPEWA TARAKA YAKE NA MAHAKAMA SOON ..... NA MALI ZAKE ANAPEWA TAKRIBAN 70% NYUMBA YA MADALE ALIYO WEKA JASHO LAKE NA BAADHI YA VITU WALIVYO CHUMA ...!!LEO πŸ˜‚πŸ˜‚ YATACHAPISHWA MAGAZETI INSTA STORY KAMA MWEHU KAKA YENU πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸƒπŸƒ."