Najua mtaniombea kifo-Amber Ray asema baada ya kulazwa hospitali

Alinukuu picha kwa kusema kuwa maadui zake na watu wa kijiji ndio chanzo kikuu.

Muhtasari
  • Amber aliendelea kusema kuwa daktari alimwambia kuwa ana maambukizi ya damu lakini daktari alimhakikishia kuwa mtoto yuko sawa

Mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu  Amber Ray amelazwa hospitalini.

Amber kupitia ukurasa wake wa  Instagram alipakia ideo akiwa kwenye kitanda cha hospitali.

Alinukuu picha kwa kusema kuwa maadui zake na watu wa kijiji ndio chanzo kikuu.

Amber aliendelea kusema kuwa daktari alimwambia kuwa ana maambukizi ya damu lakini daktari alimhakikishia kuwa mtoto yuko sawa.

Aliendelea kuwaambia watu wa kijiji chake na maadui wasimfanyie mazoezi.

Amber aliandika hivi,

"Watu wa kijiji changu na maadui wamejaribu moyo wangu wakapata ni mawe. Sasa wameona ugongwa ndo utaniweza. Anyway daktari amesema ni maambukizi ya damu lakini mtoto yuko sawa, na tafadhali msiniombee coz najua wengi wenu mtaniombea kifo. Ila nimelindwa na Mungu. ."

Haya yanajiri siku chache baada ya mpenziwe kuweka wazi kwamba wawili hao hawajaachana,ila wamekuwa wakipitia misukosuko kwenye uhusiano kama uhusiano mwinginewowote.