Kajala aonekana akipigwa busu na mwimbaji miezi baada ya kutengana na Harmonize (+video)

"Raha sana. Mwanamke mzuri sana. Wenye makasiriko wakasirike tu," alisema.

Muhtasari

•Mama huyo wa binti mmoja alipata mapokezi makubwa wakati alipowasili katika nchi hiyo jirani wa Tanzania.

•Champagne alisema kukutana na Kajala kulimpa raha sana huku akiwasuta wote ambao wangejisikia vibaya.

Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Aliyekuwa mpenzi wa staa wa Bongo Harmonize, muigizaji Frida Kajala Masanja yuko nchini Burundi kwa ziara ya kikazi.

Kajala aliwasili mjini mkuu, Bujumbura siku ya Jumanne kabla ya sherehe ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika  Jumatano katika  Safari Gate ambapo amealikwa kama mgeni maalum.

"Burundi, niko mjini. Tukutane kesho  Safari Gate tuje tusherehekee siku ya wanawake duniani. Mimi nitakuwa pale na mama zangu, dada zangu, wadogo zangu tusherehekee siku yetu muhimu sana," alisema siku ya Jumanne.

Mama huyo wa binti mmoja alipata mapokezi makubwa wakati alipowasili katika nchi hiyo jirani wa Tanzania.

Miongoni mwa watu waliomkaribisha ni pamoja na mwanamuziki maarufu Mista Champgane ambaye alionekana akimbusu baada ya kuteremka kwenye gari.

"Kajala ashafika. Ni mwanamke mzuri sana. Wenye kukasirika wasitupe mawe. Basi nisiwe na wasiwasi," Mista Champagne alisema kabla ya kumpiga mpenzi huyo wa zamani wa Harmonize busu nzuri la shavu.

Champagne alisema kukutana na Kajala kulimpa raha sana huku akiwasuta wote ambao wangejisikia vibaya.

"Raha sana. Mwanamke mzuri sana. Wenye makasiriko wakasirike tu," alisema.

Kajala alitangaza kuvunjika kwa mahusiano yake ya miezi kadhaa na bosi wa Konde Music Worldwide mapema mwezi Desemba.

Ingawa hakuweka wazi kilichowatenganisha, alisema hakubeba kinyongo dhidi ya mwimbaji huyo licha ya mahusiano kugonga mwamba.

Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema mwezi Desemba.

Mama huyo wa binti mmoja aliweka wazi kwamba alikuwa tayari kupiga hatua nyingine baada ya mahusiano kusambaratika.

Wawili hao walikuwa wamerudiana mapema mwaka jana baada ya kuwa wametengana kwa takriban mwaka mmoja.

Mahusiano yao ya kwanza yaliisha Aprili 2021 huku Harmonize akidaiwa kujaribu kumtongoza bintiye Kajala, Paula.