MCA Tricky awekwa chini ya shinikizo la kuoa

Alisema anachumbiana lakini bado hajamtambulisha mpenzi wake kwa mama yake.

Muhtasari

•Katika mahojiano na Word Is, mchekeshaji huyo alisema mama yake hataki kusikia kitu kingine chochote mwaka wa 2023.

•"Lazima niwe na uhakika kabla ya kumtambulisha kwa mama yangu," alisema

Image: INSTAGRAM// MCA TRICKY

Mchekeshaji MCA Tricky yuko chini ya shinikizo la kuoa na kupata watoto.

Katika mahojiano na Word Is, mchekeshaji huyo alisema mama yake hataki kusikia kitu kingine chochote mwaka wa 2023.

Alisema anachumbiana lakini bado hajamtambulisha mpenzi wake kwa mama yake.

"Lazima niwe na uhakika kabla ya kumtambulisha kwa mama yangu," alisema na kuongeza kuwa anapanga kutulia mwaka huu baada ya kutimiza miaka 30.

"Mama yangu ananikasirikia kwa sababu anadhani ninapaswa kuwa na watoto watatu.

"Sitafichua mengi kwa mashabiki wangu, hata baada ya kuweka mambo rasmi.

MCA Tricky anatangaza shoo yake ijayo, 'A Tricky Comedy Circuit', itakayofanyika Nairobi Cinema mnamo Machi 31.