Mke amtafutia mumewe mwanamke anayemfanana ili asi'cheat, asema hilo liliokoa ndoa

Mwanamke huyo alisema hakutaka kuvunja ndoa yake kwa sababu, “Namtaka maisha yake yote. Chochote anachotaka, chochote kinachomfurahisha, nitampa.”

Muhtasari

• Mwanamke huyo alisema hakutaka kuvunja uhusiano wake kwani alikuwa anataka kuishi na mumewe maisha yake yote.

• Hivyo alipata wazo la kumtafuta mwanamke anayemfanana mitandaoni katika kile alisema ndio mume wake anapenda.

mke aliyemtafutia mumewe mwanamke anayemfanana.
mke aliyemtafutia mumewe mwanamke anayemfanana.
Image: Screengrab

Mwanamke mmoja amegonga vichwa vya habari baada ya kudai kwamba alilazimika kumtafuta mwanamke anayemfanana kwa ajili ya kuolewa na mume wake kama mke wa pili ili kuokoa ndoa yake.

Kulingana na jarida la New York Post, mwanamke huyo kwa jina Tehmeena Quintana alivunjika moyo baada ya mume wake kwa jina Bryant Quintana kuchepuka nje ya ndoa na mwanamke mwingine, miaka 3 tu baada ya kuoana.

Hili lilimshurutisha kutafuta suluhu la haraka kwani hakutaka kuvunja uhusiano wake. Wazo likamjia kuwa ni kumtafuta mwanamke ambaye anafanana na yeye kwa kiasi kikubwa ili kuzuia macho ya nje ya mume wake.

"Zamani, Bryant hakuwa mwaminifu," Tehmeena alidai kwenye kipindi cha televisheni cha mtandaoni "Love Don't Judge."

"Ninahisi kwamba ikiwa uko na mwanamume, unapaswa kufanya chochote kinachohitajika kufanya kazi hiyo," aliendelea. “Namtaka maisha yake yote. Chochote anachotaka, chochote kinachomfurahisha, nitampa.”

Mwaka jana, Tehmeena aligeukia mitandao ya kijamii kutafuta mtu anayefanana naye ili ajiunge naye na Bryant kwenye uhusiano wa kimapenzi.

“Nilihisi kutokuwa salama tulipokuwa tukitafuta wa tatu,” mke huyo aliyejitolea akakiri. “[Lakini] nilijua kwamba ingeweka usikivu wa Bryant hapa. Ni sawa kusema kwamba nilikuwa nikitafuta msichana anayefanana nami kwa sababu Bryant anapenda hivyo.”

Hatimaye Tehmeena aliungana na mwanamitindo wa Australia Kyrah Johnson, ambaye alifanana naye kwa njia isiyo ya kawaida.

Kyrah alishawishiwa na wazo la kuwa katika kundi la watu wengi na hivi karibuni akaruka hadi New York kukutana na Tehmeena na Bryant.