Mwanasosholaiti Amber Ray amethibitisha kuwachana na mpenzi wake Kenny Rapudo.
Katika mtandao wa Instagram, Amber Ray alisema kuwa amewacha mapenzi,alisema kuwa ni siku mpya kwake kama mama kapera wa wana wawili.
Amber Ray na Kenny Rapudo walitangaza mahusiano yao kwa umma Juni mwaka wa 2022 ila uhusiano wao umekuwa na vipindi .Agosti 2022, Amber Ray alisema kuwa yeye na Kenny Rapudo hawakuwa wanachumbiana tena pamoja tena.
Oktoba 2022,wawili hao walizua hisia mseto dadake alipoweka picha ya wawili hao wakiwa kwenye karamu ya kiasili huku akiwapongeza kwa kuunganishwa kwao.Hata hivo,Ray alisema kuwa karamu hiyo ilikuwa ni Kennedy akijitambulisha kwa wazazi wake.
Rapudo alimpa ombi la ndoa Amber Ray Novemba mwaka uliopita kisha wawili hao wakaenda likizo Dubai.
Amber Ray amekuwa katika mahusiano kadhaa ikiwemo yeye na Brown Mauzo mwaka wa 2019 kisha baadaye waliwachana .Baada ya hiyo ,Mauzo alichumbiana na Vera Sidika huku Amber Ray akichumbiana na Mwanabiashara Jimal Rohosafi ambaye waliwachana tena baada ya muda . Amber aliingia kwenye mahusiano na mchezaji wa basket ball Idd Kelba baadaye.
Amber Ray ana mtoto wa miaka 11 mmoja na mpenzi wake wa zamani,akichumbiana na Kenny Rapudo,alitangaza kuwa anamtarajia mwana wake pili na hata hivi majuzi alihusika katika ugomvi mkali kati yake na Vera Sidika.
Sidika alidai kuwa Ray alinakili wazo lake la kutambulisha jinsia ya mwana wao huku Amber Ray akisema kuwa Vera Sidika anaishi maisha yasiyo yake na kwamba anafadhiliwa.
Baadhi ya watu walijibu habari hizo kama vile Oga Obinna
"Waah, rudi tu soko kama kanjo, watoto tutalea," alisema Obinna.