logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wajesus wafunguka kuhusu Akothee kuwalipa mamilioni wapambe harusi yake

Kulingana na kadi hiyo, bei za kuwashirikisha wanandoa hao katika harusi ni kati ya 125,000 hadi 3,000,000.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri12 April 2023 - 07:20

Muhtasari


•Kabi Wajesus aliweka wazi kwamba walipamba harusi hiyo kwa hisani kwani Akothee ni rafiki yao wa karibu.

•Kulingana na kadi hiyo, bei za kuwashirikisha wanandoa hao katika harusi ni kati ya 125,000 hadi 3,000,000.

Mtumbuizaji Peter Kabi wa The Wajesus Family ameweka wazi kwamba hakuna pesa zozote alizolipa mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee ili yeye na mkewe Millicent Wambui kuwa wapambe kwenye harusi yake.

Akothee na mume wake Denis Schweizer almaarufu Omosh walifunga pingu za maisha siku ya Jumatatu, Aprili 10, katika hafla ya harusi ya kupendeza iliyofanyika katika Windsor Golf Hotel & Country Club, jijini Nairobi.

Kabi na Milly walikuwa miongoni mwa watu mashuhuri walioteuliwa kupamba harusi hiyo ya pili ya mwanamuziki huyo. 

Akizungumza Jumanne, Kabi alisema ilikuwa ni heshima kubwa yeye na mke wake kuteuliwa kupamba harusi hiyo na kuweka wazi kwamba walifanya hivyo kwa hisani kwani Akothee ni rafiki yao wa karibu.

"Bado ninapata nafuu kutokana na harusi nzuri ya Akothee. Ilikuwa heshima kubwa kuwa kwenye kikosi  alafu nimepigiwa simu na KRA kwa sababu ya rate card ya @millywajesus," alisema kwenye Instagram.

"Kuweka mambo wazi, hii ya Akothee hatukulipwa . Yeye ni rafiki yetu wa kibinafsi tukianza kulipwa lazima tulipe kodi."

Kabi alilazimika kuweka mambo wazi baada ya mke wake Milly kuchapisha kadi iliyoonyesha pesa wanazotoza ili kupamba harusi.

Katika kadi hiyo ya bei, mama huyo wa watoto wawili alidokeza angefanya mengi katika harusi aliyoalikwa kwa bei fulani.

"Kuhusu mimi, ninafurahisha kwenye harusi, nakuja na mume mpenda karamu, navaa vizuri, niko na timu ya binafsi ya glam, uwepo mkubwa mtandaoni na mimi ni mcheza dansi mzuri sana," Milly aliandika kwenye kadi.

Kulingana na kadi hiyo, bei za kuwashirikisha wanandoa hao katika harusi ni kati ya 125,000 hadi 3,000,000.

Kabi alidai kwamba mkewe aliamua kuwa na bei ya malipo ya kushirishwa kwenye harusi baada ya kupamba ya Akothee.

"Yaani baada ya kusimamia harusi ya Akothee, Milly Wajesus ameamua kukuwa na rate card. Je, bei ziko sawa," aliandika.

Harusi ya pili ya Akothee iliyofanyika siku ya Jumanne ilipambwa na wanafamilia, marafiki wa karibu, wasanii maarufu na wanasiasa mashuhuri nchini. Jumla ya watu wasiopungua 300 walikuwa wamealikwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved