logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rapudo ashindwa kuficha upweke, adokeza kum'miss Amber Ray baada ya kuonekana na Jimal

Rapudo ameonyesha dalili za upweke nyumbani wiki kadhaa baada ya kutengana na Amber Ray.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri14 April 2023 - 07:25

Muhtasari


•Amber Ray na Rapudo walithibitisha kuvunjika mahusiano yao mwezi uliopita baada ya kuchumbiana kwa miezi kadhaa.

•Wikendi, Amber Ray na Jimal walizua gumzo baada ya picha  zao wakiwa kwenye hafla ya kandanda kusambazwa.

Mfanyibiashara Kennedy Rapudo ameonyesha dalili za kum'miss aliyekuwa mpenziwe, Amber Ray wiki kadhaa baada ya wawili hao kutengana.

Wazazi wenza hao watarajiwa walithibitisha kuvunjika mahusiano yao mwezi uliopita baada ya kuchumbiana kwa miezi kadhaa.

Siku ya Alhamisi, Rapudo, kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram alichapisha video fupi inayomuonyesha akitazama video ya wimbo wa Willy Paul 'Chocolate' ambao Amber Ray alihusika kama vixen.

Sehemu ya video aliyochagua kuchapisha ni ambapo mpenzi  huyo wake wa zamani alionekana kwenye skrini mara kadhaa. Pia ni sehemu ambayo mwimbaji Willy Paul aliusifia urembo wa mwanasoshalaiti huyo.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mama huyo wa mvulana mmoja kuonekana pamoja na aliyekuwa mpenzi wake, Jimal  Rohosafi. Wikendi, wawili hao walizua gumzo kubwa kwenye mitandao wa kijamii baada ya picha na video zao wakiwa kwenye hafla ya kandanda katika uwanja wa Huruma  kusambazwa.

Wapenzi hao wa zamani walionekana wakicheka pamoja huku wakiwa wameketi kando ya mwingine.

Jimal alionyesha jinsi siku yao ilivyokuwa  kwenye video na kuandika, "Kazi imekamilika. Mengi zaidi yanakuja.#jimalfoundationcup."

Amber Ray alithibitisha mwisho wa mahusiano yake na Rapudo mwishoni mwa mwezi jana kupitia mtandao wa Instagram.

Katika chapisho lake, mama huyo wa mvulana mmoja alitangaza kwamba yuko single huku akibainisha kuwa amechoshwa na mapenzi.

"Ni siku mpya ya kuanza kama mama single wa watoto wawili. Nimechoka na mapenzi," Amber Ray alisema.

Aliongeza, "Ni asubuhi, giza itaingia."

Rapudo alisema kwa upande wake hangefichua mengi lakini akaweka wazi kuwa ukweli utajidhihirisha hivi karibuni.

Katika taarifa yake, alidokeza kuwa kuna uwongo fulani ndani ya mahusiano yake  na mwanasosholaiti huyo maarufu.

"Uongo una tofauti nyingi, ukweli hauna hata moja. Katika muda usiozidi miezi miwili, sote tutajua ukweli na sababu ya kuvunjika kwa mahusiano. Ni hayo tu kwa sasa," mfanyibiasha huyo alisema mwezi uliopita.

Hapo awali, wawili hao walikuwa wameachana kwa muda mfupi na kuacha kufuatiliana kwenye Instagram. Rapudo wakati huo alisema walikuwa wakikabiliana na panda shuka kama mahusiano mengine yoyote.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved