Lulu Hassan ammiminia sifa Rashid Abdalla siku yake ya kuzaliwa

Lulu Hassan ni mtangazaji mwenza wa Rashid Abdalla katika runinga ya Citizen.

Muhtasari

• Rashid Abdalla na Lulu Hassan ni wanandoa na wana watoto 3 pamoja.

Lulu Hassan amtakia kheir ya kuzaliwa mumewe, Rashid Abdalla.
Lulu Hassan amtakia kheir ya kuzaliwa mumewe, Rashid Abdalla.
Image: INSTAGRAM// RASHID ABDALLA

Mtangazaji Lulu Hassan amwemwandikia mumewe   Rashid Abdalla maneno ya sifa katika siku yake ya kuzaliwa .

Lulu Hassan pia ni mtangazaji mwenza wa Rashid Abdalla katika programu ya Nipashe. Katika ukurasa wake wa Instagram, Lulu Hassan alieleza kuwa Rashid ana umuhimu sana katika maisha yake na kwamba ndiye kama baba ambaye hakufanikiwa kupata.

"Happy birthday mtu wangu,bosi wangu, baba ya watoto wangu. Mungu akupe umri mrefu na afya njema , wewe ni wa maana sana kwa maisha yangu, Mungu anajua. Wewe ni kama baba ambaye sikuwa naye rafiki yangu na mtu wangu. Mungu akulinde Rash, akupe hitaji la moyo na dua zako ndani ya mwezi huu mtukufu," alichapisha Lulu Hassan.

Rashid Abdalla alisherehekea siku yake ya kuzaliwa  siku ya Jumatatu.

"Mwenyezi Mungu nakuomba  uwape ufanisi wa kupitiliza, afya njema na ngekewa.Kwani wote wamekuwa nguzo muhimu katika maisha yangu. Kheir ya kuzaliwa kwangu," alisema Rashid

Lulu Hassan na Rashid Abdalla ni watangazaji wa runinga ya Citizen .Wawili hao ni wanandoa na wamebarikiwa na watoto watatu.