Davido adaiwa kuachwa na mkewe kwa kupata mtoto mwingine na baby mama wake

Kuna madai zaidi kwamba Davido alijaribu kumpa mwanamke huyo shinikizo la kutoa mimba hiyo.

Muhtasari

•Mwanamke huyo anaishi Atlanta, Marekani ambako Davido amekuwa akitembea mara kwa mara katika ziara zake za Marekani.

•Chanzo sasa kinadai Amanda tayari amejifungua mtoto, na Chioma amemuacha Davido kwa mara nyingine tena

Davido alikuwa na mwanawe Ifeanyi na mpenzi wake Chioma Rowland miaka mitatu iliyopita
Image: BBC

Mwimbaji David Adedeji Adeleke, anayejulikana kitaaluma kama Davido, anavuma mtandaoni. Anadaiwa kumpa ujauzito mpenzi wake mwingine anayeitwa Amanda anayeishi Marekani.

Kulingana na ripoti, mwanamke huyo ambaye ana mtoto mwingine naye anaishi Atlanta, Marekani ambako Davido amekuwa akitembea mara kwa mara katika ziara zake za Marekani.

Muda wa kuzaliwa kwa mtoto huyo ndio umewafanya wanamitandao kuonesha hasira. Inadaiwa ilitokea alipokuwa akifunga ndoa na Chioma wakati wote walikuwa na majonzi ya kifo cha mtoto wao.

Kuna madai zaidi kwamba Davido alijaribu kumpa mwanamke huyo shinikizo la kutoa mimba hiyo.

Kulingana na mdau wa ndani, Davido alisafiri kwa ndege hadi Amerika katika miezi ya mwanzoni mwa mwaka jana ili kutumia wakati mwingi na Amanda na binti yake wakati yeye na Chioma walikuwa wameachana.

Walakini, baada ya kifo cha Ifeanyi, familia ya Chioma ilisisitiza amuoe ili kuweza kumzika mwana wao.

Chanzo sasa kinadai Amanda tayari amejifungua mtoto, na Chioma amemuacha Davido kwa mara nyingine tena. Watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonyesha kukerwa baada ya kujua kuwa Davido amemfanyia Chioma yote hayo.

Msanii huyo amejibu katika ujumbe wa kimafumbo kwenye akaunti yake ya Twitter. Tetesi za kuenda nje ya ndoa zilimfanya aandike

"Juu ya watu wote."