"Yeye ni kijana mdogo!" Kajala afichua sababu ya kumtema Harmonize, kwa nini alirudiana naye

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alisema Harmonize huenda alihitaji nafasi ya kufanya mambo yake binafsi.

Muhtasari

•Kajala alidokeza kwamba Harmonize bado hakuwa tayari wakati alipoamua kutulia naye kwenye mahusiano.

•Kajala alibainisha kwamba alikubali kurudaina na bosi huyo wa Konde Music Worldwide kwa kuwa bado alimpenda.

Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Muigizaji maarufu wa filamu Bongo Frida Kajala Masanja hatimaye ameweka mambo wazi kuhusu kutengana kwake na Harmonize.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha redio cha hapa nchini, alidokeza kuwa alimtema mwimbaji huyo kwa sababu ya mazoea.

"Sijui niseme nini. Labda mazoea. Mtu akishakuzoea sana anakuchukulia poa," alisema.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alidokeza kwamba Harmonize bado hakuwa tayari wakati alipoamua kutulia naye kwenye mahusiano na kuwa huenda alihitaji nafasi ya kufanya mambo yake binafsi.

"Yaani mimi hata simlaumu, kwa sababu yeye ni kijana mdogo. Labda alihitaji nafasi, tulikuwa tuko karibu sana.

Yeye mara ya kwanza nahisi labda aliona kama mzaha akisema nataka huyu mtu, nataka niwe naye 24/7.  Mnaamka wote mnaenda gym, mnafanya hiki na kile. Labda alikuwa anahitaji nafasi yake afanye vitu vyake," alisema.

Kajala alibainisha kwamba alikubali kurudaina na bosi huyo wa Konde Music Worldwide kwa kuwa bado alikuwa anampenda.

Hata hivyo, alifichua kuwa tayari alikuwa amesonga mbele na maisha yake kabla ya Konde Boy kunyeyekea na kuomba radhi.

"Nilirudiana naye kwa sababu nilikuwa nampenda. Nilimove on, lakini ilikuwa mtu ambaye bado yupo. Alafu alipoomba msamaha nilijua.. sijui niseme nini," muigizaji huyo alisema kabla ya kukosa maneno ya kuelezea.

Mama huyo wa binti mmoja alikiri kwamba Harmonize alifanya wimbo 'Nitaubeba' maalum kwa ajili yake. Aliendelea kusifia kipaji cha mpenzi huyo wake wa zamani huku akitaja nyimbo zake kuwa nzuri.

Kajala alipoulizwa ikiwa tayari amepata mpenzi mwingine baada ya kumtema staa huyo wa Bongo, aliweka wazi amkekuwa kwenye mahusiano na mwanasiasa mashuhuri wa Kenya kwa miezi miwili sasa.

"Nimemove on na mtu. Mhusika anatoka Kenya. Ni mtu anajulikana. Ni mwanasiasa. Alianza kunitongoza  kama wengine wanavyoanza. Sasa unaenda mwezi wa pili," alisema muigizaji huyo wa filamu bongo.

Malkia huyo mrembo mwenye umri wa miaka 40 pia alisistiza kuwa yupo tayari kupata mtoto mwingine wa pili.

Wakati akitangaza kutengana na Harmonize mwishoni mwa mwaka jana, Kajala aliweka wazi kwamba alikuwa tayari kupiga hatua nyingine baada ya mahusiano yao ya miezi michache kugonga mwamba.

Ingawa hakufichua kilichowatenganisha, aliweka wazi kwamba hakubeba kinyongo chochote dhidi ya mwimbaji huyo.

"Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema mwezi Desemba.