Mwanatiktoka Shon Arwa abubujikwa na machozi baada ya kuhamia ughaibuni

Arwa alieleza wasiwasi wake kwa kuwa na lafudhi tofauti inayoweza kufanya akose kuelewka.

Muhtasari

•Ingawaja Arwa hajafichua ni wapi amehamia,alidokeza kuwa mwanawe na babake walikutana mara ya kwanza mwaka huu alipoondoka na mtoto wake kwenda ughaibuni.

Shon Arwa ahamia ughaibuni
Shon Arwa ahamia ughaibuni
Image: INSTAGRAM

Mwanatiktoka maarufu Shon Arwa alilengwa na machozi ya huzuni baada ya kuhamia  ughaibuni kufungua ukurasa mpya wa maisha .

Katika video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Arwa alilengwa na machozi akieleza wasiwasi wake kwa kuanza ukurasa mpya wa maisha katika nchi ambayo hajazoea namna ya maisha yao na asikojulikana na mtu yeyote.

"Nilitaka sana kuondoka ila nilipoondoka sikuwa na furaha kama nilivyodhania kwa sababu ukweli wa kuwa nilikuwa ninawacha kila kitu ambacho nilikuwa nimejua, kuwawacha nyuma marafiki zangu na familia yangu,ni kama mtoto anayejifunza kutembea," alisema Arwa.

Arwa aliongezea kuwa ana wasiwasi kupatana na maisha mageni kwa sababu kila kitu ni jipya,alisema kuwa mwanawe hatapata nafasi ya kulia nchini Kenya kwa sababu atakulia katika mazingira tofauti.

Ingawaja Arwa hajafichua ni wapi amehamia,alidokeza kuwa mwanawe na babake walikutana mara ya kwanza mwaka huu alipoondoka na mtoto wake kwenda ughaibuni.

Arwa alieleza zaidi kuwa anamshukuru dadake kwa kumlea kama mtoto wake huku akisema kuwa alitoka katika familia ambayo walidharauliwa kwa kukejeliwa kuwa hawawezi kufanikiwa. Alisema kuwa licha ya watu kuwaona kama wajinga darasani, walifanikiwa kufuzu shuleni kwa sababu ya dadake.

"Natoka katika familia iliyodhaniwa kuwa wajinga darasani ila Mungu amefanya kazi kupitia dadangu na tumefanikiwa kufuzu wote.

Arwa amehamia ughaibuni kwenda kuishi na mume wake ambaye wana mtoto mmoja pamoja.