logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rapudo aonyesha upendo kwa mwanawe Amber Ray licha ya kutengana

Mfanyabiashara huyo amemtakia Garvin upendo na furaha tele maishani huku akimtambua kama bingwa.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri26 April 2023 - 06:19

Muhtasari


•Rapudo amewashangaza wengi  kwa kumsherehekea mwanawe Amber Ray, Garvin mnamo siku yake ya kuzaliwa.

•Mfanyibiashara huyo aliambatanisha ujumbe huo na picha yake na Garvin wakiwa wanacheza mchezo wa gofu.

Mfanyibiashara Kennedy Rapudo na mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray wameendelea kuwachanganya mashabiki wao kuhusu uhusiano wao wa sasa baada ya kudaiwa kutengana mwezi uliopita.

Wawili hao ambao wanatarajia mtoto pamoja hivi karibuni walidaiwa kutengana mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa. Wote walitoa taarifa za kuthibitisha kutengana.

Siku ya Jumatano hata hivyo, Rapudo aliwashangaza wengi ambao wamekuwa wakifuatilia mahusiano yao kwa karibu kwa kumsherehekea mwanawe Amber Ray, Garvin mnamo siku yake ya kuzaliwa.

"Naomba upate kuzungukwa na upendo mwingi na vitu vyote vinavyokufanya utabasamu. Kheri ya siku ya kuzaliwa bingwa!" Rapudo alimwandikia mtoto huyo wa pekee wa Amber Ray kwenye mtandao wa Instagram.

Mfanyibiashara huyo aliambatanisha ujumbe huo na picha yake na Garvin wakiwa wanacheza mchezo wa gofu.

Amber Ray alithibitisha mwisho wa mahusiano yao ya miezi kadhaa mwishoni mwa mwezi jana kupitia mtandao wa Instagram.

Katika chapisho lake, mama huyo wa mvulana mmoja alitangaza kuwa yuko single huku akibainisha kuwa amechoshwa na mapenzi.

"Ni siku mpya ya kuanza kama mama single wa watoto wawili. Nimechoka na mapenzi," Amber Ray alisema.

Aliongeza, "Ni asubuhi, giza itaingia."

Kwa upande wake, Rapudo alisema hatafichua mengi kuhusu kile kilichotokea lakini akaweka wazi kuwa ukweli utajidhihirisha hivi karibuni.

Katika taarifa yake ya Instagram, alidokeza kuwa kuna uwongo fulani ndani ya mahusiano yake  na mwanasosholaiti huyo maarufu.

"Uongo una tofauti nyingi, ukweli hauna hata moja. Katika muda usiozidi miezi miwili, sote tutajua ukweli na sababu ya kuvunjika kwa mahusiano. Ni hayo tu kwa sasa," mfanyibiasha huyo alisema kwenye Instagram.

Siku chache baadaye, Amber Ray aliwashangaza wengi baada ya kuonekana na aliyekuwa mpenzi wake Jimal Rohosafi. Wawili hao walizua gumzo kubwa kwenye mitandao wa kijamii baada ya picha na video zao kadhaawakiwa kwenye hafla ya kandanda katika uwanja wa Huruma  kusambazwa.

Pichani, wapenzi hao wa zamani walionekana wakicheka pamoja huku wakiwa wameketi kando ya mwingine.

Jimal alionyesha jinsi siku yao ilivyokuwa  kwenye video na kuandika, "Kazi imekamilika. Mengi zaidi yanakuja.#jimalfoundationcup."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved