logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pritty Vishy: Usinitongoze kama wewe ni mwanaume wa kanisa

Vishy alisema kuwa anaafadhalisha kupeleka sadaka kwa watoto yatima.

image
na

Yanayojiri28 April 2023 - 06:56

Muhtasari


" Usinichukue  kama wewe ni kijana wa kanisa kwa sababu utaenda kanisani kwenu ukaambiwe nenda ukamnyonge mke wako," aliandika Vishy.

Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa

Aliyekuwa mpenzi wa rapa Stivo Simple Boy, Pritty Vishy amesema hatakubali kutongozwa na mwanaume ambaye anaenda kanisani.

Vishy, kwenye chapisho katika ukurasa wake wa Instagram, Vishy alieleza kuwa hofu ya sarakasi ya dini ambayo imezuka hivi majuzi.

"Tulikofika tafadhali kama wajua wewe ni mwanaume wa kanisa usinitongoze, kwa sababu mara Mackenzie,mara Ezekiel mara sio hii ingine amabyo sitatataja ambao wanapeleka udaku kanisani," alisema Pritty Vishy.

Aliongezea kuwa kama ni sadaka ni bora kupeleka katika vituo vya watoto yatima.

"Kama ni kuomba tutagawa nyumba yetu ili ufanye hivo na marafiki na familia yako. Kama ni sadaka na fungu tutaoa tupeleke kwa watoto yatima, usinichukue  kama wewe ni kijana wa kanisa kwa sababu utaenda kanisani kwenu ukaambiwe nenda ukamnyonge mke wako," aliandika Vishy.

Pritty Vishy alikuwa mpenzi wa Simple Boy kabla ya wawili hao kutengana. Wawili hao hata hivyo wamekuwa wakirushiana vijembe mtandaoni tangu kutengana kwao  Vishy akidai kuwa Simple Boy na mpenzi wake wa sasa Grace Otieno bado hawajaoana na kuwa wanadanganya umma kuwa wamefunga ndoa.

Vishy alifichua kuwa kwa sasa anachumbiana na mtu ila kwa faragha .Kwa upande wake simple Boy, alimtambulisha Atieno kama mke wake wakati wa mazishi ya baba yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved