logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kumekucha! Twitter kufunga akaunti zenye zimekuwa kimya kwa muda mrefu

Musk alibainisha hata hivyo kwamba akaunti hizo zitawekwa kwenye ghala na si kufutwa.

image
na Radio Jambo

Habari09 May 2023 - 09:08

Muhtasari


• Baadhi walimuunga mkono wakisema kuwa ni hatua nzuri itakayowajulisha watu ni idadi ipi ya wafuasi wanaotumia Twitter wanao.

Tajiri namba moja duniani awataka watu wazaane kwa wingi

Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Twitter Elon Musk ametangaza sasisho linguine jipya kwa watumizi wa mtandao huo.

Musk anahoji kwamba hivi karibuni watajukumika kufanyia mtandao huo usafi ili kufagia akaunti zote zisizotumika na kuzitumbukiza kwenye debe la takataka.

Musk alisema kwamba tangu achukue udhibiti na umiliki wa mtandao huo mkubwa, amekuwa akifanya udadisi na kugundua kwama kuna akaunti nyingi ambazo zimekuwa kimya kwa muda mrefu pasi na kufanya kitu chochote iwe ni kupakia, kuretweet au ku’like kitu chochote.

Alisema kuwa hizo ndizo akaunti ambazo atalenga kufagia kabisa na kuwafanyia mzaha watumizi wa mtandao huo kwamba anataka kuona furaha yake watu wakipoteza takwimu za wafuasi.

“Tunasafisha akaunti ambazo hazijakuwa na shughuli yoyote kwa miaka kadhaa, kwa hivyo huenda utaona kupungua kwa idadi ya wanaokufuata,” Musk alisema.

Baadhi walimuunga mkono wakisema kuwa ni hatua nzuri itakayowajulisha watu ni idadi ipi ya wafuasi wanaotumia Twitter wanao, na itakuwa vyema kuchunga akaunti zote ambazo hazitumiki ili kuleta uhalalai.

“Huenda ninasoma hii kimakosa, lakini ikiwa kwa hakika unafuta akaunti ambazo hazitumiki na tweets zao zote za kihistoria, ningekusihi sana ufikirie upya. Kufahamisha watu ni wangapi wanaofuata wafuasi "hai" ni taarifa nzuri, lakini kufuta matokeo ya akaunti ambazo hazitumiki itakuwa mbaya sana,” John Carmack alimsihi.

Akilijibu hili, Musk alibainisha kwamba hana nia ya kufuta kabisa bali alieleweka vibaya kwani nia yake ni kuziweka akaunti hizo kwenye ghala na si kufutwa kabisa.

Tangazo hili linafuatila lile ambalo lilipata pingamizi kali kutoka kwa watumizi wa Twitter baada ya Musk kusema kuwa yeyote mwenye anataka kuhifadhi beji ya bluu anapaswa kulipia kiasi cha dola 8 kila mwezi.

Musk alifikia hatua akaondoa beji hizo kwa akaunti zote ambazo hazikuwa zimelipia lakini baada ya watu kuteta, ilimbidi kurudisha beji hizo kwa akaunti ambazo zina wafuasi zaidi ya milioni moja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved