Dereva wa teksi atamka laana ya kifo kwa mpenziwe kwa kusema yeye si hadhi yake tena

Mwanamume huyo mwenye uchungu alifanya vimbwanga kwenye mchanga wa kaburi akivunja yai na kunyunyizia pombe kwa kile alisema alifadhili mpenziwe kusomea uuguzi lakini akamgeuka.

Muhtasari

• Dereva wa teksi alifadhili masomo ya uuguzi kwa mpenzi wake na baada ya kuhitimu, alimtema dereva huyo akisema hamfai.

• Kwa mfadhaiko, alichimba mchanga kama kaburi na kuanza kufanya vimbwanga ikiwemo kupasua yai akitamka laana ya kifo kwa muuguzi huyo.

• Katika video hiyo, mwanamume huyo aliyechanganyikiwa kihisia pia alidai kuwa mrembo wake alikuwa na mtoto alipokutana naye, lakini hilo halikumzuia kumchumbia.

Dereva wa teksi amlaani mpenziwe aliyemtoroka.
Dereva wa teksi amlaani mpenziwe aliyemtoroka.
Image: Facebok// Screengrab salty tv

Dereva wa teksi amegonga vichwa vya habari baada ya kuonekana kufanya vimbwanga kwenye mchanga katika kile kiliaminika kuwa ni kulaani mpenzi wake aliyemtoroka baada ya kujitolea kumfadhili kimasomo.

Katika video hiyo, mwanamume huyo aliyekuwa amevalia tisheti ya njano alionekana anatamka maneno kwenye mchanga kichakani akiwa ameshikilia kitu kilichoonekana kama yai mkononi.

Maelezo ya video hiyo yalifafanua kwamba Mwanamume huyo aliamua kutamka laana ya kifo kwa mpenzi wake baada ya kumsomesha kupata stashahada ya uuguzi na mwisho wa siku yule binti akarudi akimwambia kwamba yeye si wa hadhi yake na wala hamfai.

Kwa mfadhaiko na ghadhabu, mhudumu wa teksi aliamua kumpa laana ya kufa.

Kulingana na mwanaume huyo, mrembo wake alikuwa mtoro shuleni ambaye aliuza mayai chini ya jua kali ili kujikimu yeye mwenyewe, mtoto wake na wazazi wake alipokutana naye kwa mara ya kwanza.

Alimuandikisha tena shuleni na kumhudumia hadi alipohitimu.

Mrembo huyo kwa sasa ni mhitimu na amekutana na mpenzi mpya, hivyo anadai hayupo tena katika hadhi ya dereva wa teksi licha ya kujinyima kila alichokuwa nacho ili kumfurahisha.

Baada ya kumtunza shuleni, dereva wa teksi anamhukumu kifo kwa kutangaza kuwa si wa kiwango chake kimaisha tena.

Katika video hiyo, mwanamume huyo aliyechanganyikiwa kihisia pia alidai kuwa mrembo wake alikuwa na mtoto alipokutana naye, lakini hilo halikumzuia kumchumbia.

Alimtunza mtoto wa mamake pamoja na wazazi wake kwa sababu wote walitegemea biashara ya mayai yaliyouzwa ili kuishi.

Dereva wa teksi mdogo alitumia familia nzima ya mrembo huyo kama shukrani kwa miungu ambao aliwaita kumshughulikia hadi kifo, kwa niaba yake.

Tazama video hapa chini kujua zaidi.